NA TIMA SALEHE, DAR RES SALAAM

ZIKIWA zimebakia siku chache kumalizika kwa mwaka 2020 kuna matukio mbali mbali ambayo yamejitokeza mwaka huu.

Katika kila idara kumekuwa na jambo lake ikiwa lakufurahisha ama lakusikitisha, na kwakuwa mwaka unamalizika sio vibaya kama tutawakumbuka japo kwa uchache nyota ambao wamewika mwaka huu katika anga la burudani ya muziki wa kizazi kipya.

Wengi wanadhani ni rahisi ndio maana unakuta kuna wimbi la vijana na wazee ambao wanakimbilia kufanya mziki, wakiamini kwamba ndio sehemu rahisi kutoka kimaisha, lakini sio kweli, kujua na kujituma ndio nguzo pekee ya kufanya vizuri kama hujui huwezi kusikilizwa na kama unajua tuu halafu hujitumi basi huwezi kufanikiwa.

Kiukweli Tanzania imebarikiwa kuwa na wanamuziki wengi ambao kila kukicha wana konga nyoyo za mashabiki wao na kuing’arisha nchi hata nje ya mipaka yetu.

Nchi tofauti tofauti zimekuwa zikitamani hata kuwa miliki baadhi ya nyota  kutokana na ubora wa kazi zao jambo ambalo hata watanzania wenyewe wanajivunia.

Hawa ni baadhi ya wasanii wachache kati ya  wengi ambao tangu mwaka unaanza wanafanya vizuri na kuiwakilisha vizuri nchi.

DAIMOND PLATNUMZ

DIAMOND-PLATNUMZ

Haitakuwa vibaya kuanza na Diamond Platnums, ambae hivi karibuni ameachi ngoma yake ya ‘Waaa’ ambayo’ amemshirikisha msanii mkongwe kutoka Congo  Koffie Olomide, Tangu mwaka umeanza Daimond ama Simba amekuwa yupo vizuri  na kila mtu amekuwa hana deni kwake kutokana na kazi nzuri ambayo anaifanya

Daimond hivi karibuni alipata tunzo ya msanii bora wa kiume Afrika.

MARIOO

MARIOO

Msanii Mario amekuwa akifanya vizuri wakati wote na wakati mwingine hata kuwatungia watu nyimbo, ambazo baadae huwa hawafichi kuwa kijana huyo ndio aliye watungia nyimbo hizo, na nyimbo yake ambayo kwasasa inatamba zaidi ni Mama Amina aliyoifanya nchini Afrika Kusini na kuwashirikisha Sho Madjozi na Bontle Smith Wasanii kutokana nchini huko.

ALI KIBA,

ALI KIBA

Ali Kiba ni msanii ambaye alifanya vizuri kutokana na harakati ambazo amekuwa akizifanya kuhakikisha watu hawa msahaua, mpaka sasa wimbo ambao unambeba ni ‘Mediocare’.

NANDY

NANDY

Nandy amekuwa bora miongoni mwa wasanii wengi wa kike ambao wanafanya kazi ya muziki Tanzania, sio vibaya kusema anaweza kuwa mfano wa kuigwa kutokana na juhudi anazo zifanya kuhakikisha muziki wake unakuwa, na hiyo imemfanya kupata tuzo ya msanii bora wa kike Afrika zilizo tolewa AFRIMMA mwaka huu,

Hivi karibuni Nandy ameachi ngoma yake ambayo amemshirikisha mkongwe Ali  Kiba inayotamba  kwa jina la Nibakishie.

HARMONISE

HARMONISE

Mmoja ya watu muhimu kwenye muziki Tanzania na hivi karibuni ameachia wimbo wake unao kwenda kwajina la Ushamba,

Haukuwa mwaka mbaya kwake na huku ukingoni pia anaumaliza vizuri, watu wengi hawakudhani kwamba msanii huyu angeweza kuhimili kufanya kazi pekeyake baada ya kutoka kwenye lebo ya Wasafi, lakini imekuwa tofauti mwaka huu ameweza kuachia Album yake ambayo bado inafanya vizuri mpaka sasa.

ZUCHU

ZUCHU

Msanii chipukizi kutoka kwenye lebo ya wasafi, amekuwa akifanya vizuri sana nchini Tanzania na kazi zake zina sikilizwa sana ndani na hata nje tukiwa kwenye mwisho wa mwaka ameachia wimbo ambao ame mshirikisha Diamond kwajina la Cheche, ni moja ya nyimbo ambazo zinafanya vizuri sana kwenye soko la muziki ndani na hata nje.

Zuchu amefanya ngoma nyingi kwa muda mfupi na kufanikiwa kupata tuzo ya msanii bora wakike chipukizi Afrika

MEJA KUNTA

MEJA KUNTA

Meja ni  mmoja ya wasanii Chipukizi wa muziki wa Singeli ambao kila mmoja anafurahia kazi zake kwa muda mfupi, aliweza kuwika nakazi yake ya mamu ambayo mpaka sasa inafanya vizuri sambamba na nyimbo zingine ambazo zinaendelea kufanya vizuri nakumpa umaarufu kwa mwaka huu 2020.

MAROMBOSO

MAROMBOSO

Muhindi wa Kusini hupenda kujiita hivyo wimbo wa mwisho ambao ameuachia mwaka huu na unafanya vizuri niu Dear X, Maromboso ni moja ya wasanii pendwa Tanzania na wanafanya vizuri,

Ndani ya mwaka huu ameachia kazi nyingi ambazo zimemfanya kutoka kwenye vichwa vya wapenda muziki mzuri hiyo yote ikichagiwa na mashairi  mazuri ambayo mwanamziki huyu amekuwa akiyatumia kuwafanya wapenzi wa mziki kumsikiliza.

IBRAH            

IBRAH

Msanii kutoka kundi la ‘Konde Gang’, ambaye ametambulishwa mwaka huu nakuanza kuachia kazi zake ambazo zimemtengenezea jina nakufanya akubalike mpaka sasa.