LONDON, England
HUKU nusu ya kwanza ya msimu wa 2020-21 wa Ligi Kuu ya England ukikaribia kumalizika, klabu zinazoshiriki ligi hiyo bila ya shaka zimeanza kutafakari ni wapi vikosi vyao vinahitaji kuimarishwa.
Je ni wachezaji wapi watakuwa katika orodha ya mameneja wa ligi kuu?

ARSENAL

Arsenal wanahitaji ubunifu na msukumo kutoka mahali pengine kwani wale walioletwa mpaka sasa baadhi yao wamejeruhiwa (Thomas Partey) au hawajaleta mabadiliko makubwa (Willian) hii ni baada ya klabu hiyo kuanza msimu kwa kuandikisha matokeo mabaya.


Kiungo wa kati wa zamani wa Tottenham Christian Eriksen, ambaye aliangushwa na Inter Milan, anapigiwa upatu kusajiliwa na klabu hiyo, Kwani kumpata Houssem Aouar kutoka Lyon, mwezi Januari itakuwa kibarua kigumu.Emi Buendia wa Norwich pia huenda akawa mmoja wa wachezaji ambaye yuko katika kiwango cha bei ya Arsenal.Meneja, Mikel Arteta ameahidiwa usaidizi na mkurugenzi wa kiufundi Edu na mahesabu yanapigwa.

Wakati Arsenal inapoangalia bajeti yake na kujitathmini, Je hatimaye watafanikiwa kumuondoa Mesut Ozil katika bili yao ya mshahara mwezi Januari?.

CHELSEA

Inafahamika wazi ni mchezaji gani ambaye meneja wa Chelsea Frank Lampard angelipenda ajiunge na kikosi chake, lakini, anachotaka na kile atakachopata huenda ikiwa vitu viwili tofauti katika soko la Januari.Lampard angelipendelea kumsajili Declan Rice, kiungo wa kati ambaye ana uwezo wa kuwa mlinzi wa kati, lakini, je West Ham wanapanga kumuuza Januari?

Bila ya shaka, hilo huenda lisifanyike.Chelsea na Lampard watalazimika kusubiri na kuelekeza darubini yao katika kuwaondoa baadhi ya wachezaji katika bili yao ya mishahara, kama Antonio Rudiger, Andreas Christensen na Marcos Alonso.

CRYSTAL PALACE

Usitarajie usajili wa hali ya juu kutoka kwa meneja wa Crystal Palace, Roy Hodgson. Kuna hata uwezekano wa kukomeshwa kwa uvumi usiokuwa na mwisho unaomzunguka Wilfried Zaha, aliyehusishwa na kuondoka klabu hiyo tukio ambalo halikufanyika.

EVERTON
Mkurugenzi wa soka wa Everton, Marcel Brands sio shabiki wa kununua wachezaji Januari, lakini, meneja Carlo Ancelotti huenda akataka kuimarisha kikosi chake ambacho baadhi ya wachezaji ni majeruhi, lakini, kinatazamia kuwa imara nusu ya pili ya msimu.

Msimu iliyopita, Ancelotti, alikuwa anataka kuimarisha beki ya kulia, lakini, majina makubwa ya wachezaji waliokuwa karibu na Mtaliano huyo alipokuwa Real Madrid yametajwa.
Wachezji hao ni Isco, ambaye bado yuko Bernabeu na Sami Khedira, kiungo wa Ujerumani ambaye yuko Juventus, na aliyekiri kuwasiliana na meneja wa Everton.

Demarai Gray Leicester pia anapigiwa upatu kuhamia Goodison Park, huku jina la Dele Alli wa Tottenham pia likitajwa.Mchezaji wa safu ya mashambulizi huenda akapewa kipaumbele endapo klabu hiyo itaamua kusamsajili mchezaji mpya, lakini, itategemea na kuondoka kwa Cenk Tosun, kwani kubana matumizi kunasalia kuwa lengo kuu.

LIVERPOOL

Moja ya suali kuu hapa ni iwapo, meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp, atawatafuta wachezaji wa kushikilia nafasi za Virgil van Dijk na Joe Gomez? Wawili hao wanauguza jeraha la goti na huenda wasicheze tena msimu huu.

Klopp atachukuwa hatua hiyo akiwa na uhakika asilimia 100 ikiwa hatua hiyo ina muafaka kwa Liverpool na wala sio suluhisho la muda mfupi au hatua ya mbadala.

Kufikia sasa, ushirikiano wa Fabinho, Joel Matip na wachezaji chipukizi kama Rhys Williams umeiwezesha Liverpool kuongoza msimamo wa ligi kwa mara nyengine.

Liverpool wamehusishwa na uhamisho wa Ozan Kabak wa Schalke na mlinzi wa Lille, Sven Botman, lakini, uzoefu wa zamani unaashiria Klopp atafanya uamuzi kwa umakini. Atahakikisha usajili wowote wa mchezaji mpya utakuwa na manufaa makubwa kwa kikosi chake.Shujaa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati waliposhinda taji hilo mwaka 2019, Divock Origi, huenda akaondoka klabu hiyo.

MANCHESTER CITY

Inaonekana Januari hued ikawa kimya katika uwanja wa Etihad, ijapokuwa, Pep Guardiola huenda akashawishika kutaka kuimarisha safu yake ya kati na nyuma. Benjamin Mendy amekuwa akijeruhiwa mara kwa mara naye Oleksandr Zinchenko sio mzuri vile.
Kuangalia mbele zaidi, ManCity na Guardiola watahitajika kupanga mikakati bila ya Sergio Aguero.

MANCHESTER UNITED

Ole Gunnar Solskjaer anataka kuimarisha ulinzi wa safu yake ya kati ili kujiweka katika nafas nzuri ya kufanya mashambulizi. Bila ya shaka anatazamiwa kufanya hilo mwezi Januari.


Licha ya kwamba Jadon Sancho wa Borussia Dortmund na England anasalia kuwa lengo la muda mrefu. Wachezaji wanaopigiwa upatu kushikilia nafasi hiyo ni pamoja na Dayet Upamecano wa RB Leipzig

ambaye hatategemewa na klabu hiyo ya Bundesliga katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ben White wa Brighton.Hata hivyo, Solskjaer anatarajia kukamilisha usajili wa winga, Amad Diallowa wa Atalanta kwa pauni milioni 19.

TOTTENHAM HOTSPURS

Kwa Tottenham, suali kuu la Januari ni ikiwa Dele Alli, aliyetengwa na Jose Mourinho, atasalia katika klabu hiyo mwisho wa mwezi huo, huku Paris St-Germain ikiwa bado imeonesha nia ya kutaka kumnunua.

Mourinho amehusishwa na mango wa kutaka kumnunua kiungo wa kati matata wa Juventus, Sami Khedira, lakini mjadala huenda ukamzunguka Alli, ambaye nyota yake imefifia tangu alipotangazwa kuwa mchezaji mahiriwa wa England wa siku zijazo.

ASTON VILLA

Klabu hii haitarajiwi kutumia fedha nyingi kununua wachezaji wapya lakini meneja Dean Smithhuenda akaamua kuangazia darubini yake katika safu ya mashambulizi.

Ollie Watkins, ambaye alisajiliwa kwa pauni milioni 28 kutoka Brentford, amekuwa akifanya kazi nzuri, lakini, Keinan Davis hajafunga mabao ya kutosha alipokuwa na nafasi hiyo.Januari sio soko zuri la kununua bidhaa iliyo na thamani kama ya magoli, kwani Villa ilifahamu hilo kwa njia ngumu baada ya usajili wa pauni milioni 8.5 kutoka Genk mwaka jana.

Kwa sasa yuko Fenerbahce kwa mkopo.Villa kwa muda mrefu wamekuwa wakimnyatia Milot Rashica wa Werder Bremen, lakini, hawana mpango wa kutumia fedha za kisawasawa.