BUENOS AIRES, Argentina

WAFANYAKAZI waliohusika katika mazishi ya gwiji wa soka Diego Maradona wameomba msamaha, baada ya kupiga picha na mwili wa marehemu ukiwa kwenye Jeneza.

Tayari Wafanyakazi hao wamefukuzwa kazi lakini wanalalamikia kuwa raia wenye hasira kali wanawatishia kuwaua kutokana na kitendo hicho.

Claudio Fernandez ambaye alipiga picha pembeni ya Jeneza la Maradona akiwa na mwanawe, pamoja na mwanamme mwingine ambaye aliushika kabisa mwili na kupiga picha, wameomba radhi na kusema walifanya hivyo kwa upendo wao tu kwa marehemu