KIGALI,RWANDA

KIKUNDI cha wakimbizi na waomba hifadhi 130 kutoka Libya wamefiki Rwanda Desemba 29, na kuwa kundi la tano kutoka nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika kukaribishwa kwa muda nchini Rwanda.

Watafuta hifadhi hao watahamishwa katika nchi nyengine, kulingana na mpangilio uliopo.

Kulingana na UNHCR, shirika la wakimbizi ulimwenguni, kundi hilo linajumuisha Waeritrea 67, Wasudan 48, Wasomali 12, Wanigeria wawili, na mmoja wa Libya.

Inaonekana,wengi wa waliofika hivi karibuni ni vijana, na wenzi wachache ambao walikuwa na watoto wao wadogo.

Walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali, walipimwa Covid-19 na baadaye walipelekwa Hoteli ya La Palisse Nyamata wilayani Bugesera kutoka ambapo watasubiri matokeo yao.

Ilielezwa kuwa baadae wataendelea na usafiri wa dharura ya Gashora iliyoko katika wilaya hiyo hiyo, ambapo watakuwa na makaazi.

Tangu 2019, Rwanda imekuwa ikipokea wakimbizi na waomba hifadhi ambao walihamishwa kutoka Libya, baada ya kukwama huko, wengine kwa miaka.

Hatua hiyo inaambatana na mfumo uliowekwa kupitia makubaliano ya pande tatu kati ya Serikali ya Rwanda, UNHCR, na Umoja wa Afrika.

Chini ya makubaliano hayo,Rwanda ilitoa ahadi ya kuwakaribisha wakimbizi wa Kiafrika waliokwama Libya baada ya juhudi zao kubwa za kuifanya nchi za Ulaya zikatishwe.

Kwa jumla,wakimbizi na waomba hifadhi 515 hadi sasa wamehamishwa kwenda Rwanda na kati ya hao, zaidi ya 200 walipewa makaazi katika nchi nyengine haswa Ulaya.

Kulingana na Wizara ya usimamizi wa dharura,131 walipewa makaazi huko Sweden, 23 nchini Canada, 46 nchini Norway, na watano Ufaransa.