NA ASIA MWALIM

WAZAZI na walezi nchini wameshauriwa kuwapa mashirikiano watoto wao ili waweze kufikia malengo waliyo jiwekea kwa kupata elimu sahihi.

Mwalimu Mkuu wa skuli ya Heroes Community Academy Abdul rauf Mzee Rajab, alitoa wito huo wakati wa mahafali ya kwanza ya skuli hiyo huko Fuoni Uwandani Zanzibar.

Mwalimu huyo, alisema wanafunzi wanahitaji ushirikiano wa karibu kutoka kwa wazazi, ili waweze kusoma kwa bidii, na kuwafanya  kuongoza vyema katika masomo yao.

Aidha alisema utayari wa wazazi na walimu ndio utakaosaidia kufanikisha malengo husika kwa wanafunzi ambao ndio taifa la kesho na kupata  wa taalamu bora wa badae.

Alifahamisha kuwa Serekali Ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo mstari wa mbele kuimarisha sekta ya elimu sambamba na kuunga mkono juhudi za skuli binafsi nchini ili kupiga hatua ya kimaendeleo.

Alieleza kuwa Skuli ya Heroes Community Academy ilioanzishwa mwaka 2019, ikiwa na wanafunzi wakike 22 na wakiume 20 kwa madarasa ya chekechea (nursery)ambayo ipo chini ya taasisi ya Zanzibar Learning  For life  Foundation .

Hata hivyo, aliomba jamii  kushirikiana katika kulea watoto, ili kufanikisha ndoto zao  Sambamba na kupata wataalamu wa watakao leta maendeleo nchini.

Nae Halima Abushiri Abeid,  Mzazi wa mwanafunzi aliehudhuria mahafali hiyo aliwashauri wazazi kuwa peleka watoto kusoma elimu ya msingi kwani inasaidia na kuwapa muamko wanapoanza darasa la msingi.

“Masomo ya chekechea yamemsaidia mwanangu amejifunza mengi awali hakujua chochote sasa anajua kuhesabu, kusoma na kuandika kiengereza”alisema mzazi.

Skuli hiyo ipo chini ya wadhamini mbalimbali ikiwemo Daraja Foundation, Cocos Foundation, All Saints Anglican school, Zanlink Liquid Telecom,Rotary Club of Stown Zanzibar, Rotary Club of Brighton and Hove Soree My Book Buddy