NA ABDI SULEIMAN

WAZAZI wametakiwa kuwekeza nguvu zaidi katika elimu kwa watoto wao, kwani bila ya elimu hakuna kitu chochote kitakachowasaidia.

Hayo yalielezwa na mwakilishi wajimbo la Wawi, Bakar Hamad Bakar, wakati akizungumza na wazazi, walimu na wanafunzi katika mahafali ya kwanza ya skuli ya Al-jitihad Nnisai Islamiya iliyopo Kichangani wilaya ya Chake Chake.

Alisema katika miaka ya hivi karibuni wazazi wamejikita zaidi kuchangia mambo ya dunia kuliko elimu ya watoto wao.

Alifahamisha kuwa elimu ndio msingi wa maisha ya mtoto hivyo kuna haja kwa wazazi kuwekeza nguvu na mali kuhakikisha watoto wanasoma.

 “Leo mzazi yuko tayari kuchangia harusi lakini suala la kuchagia au kulipia ada mtoto wake ni tatizo,” alisema.