BLOEMFONTEIN,AFRIKA KUSINI

SHIRIKA la Afya Duniani, WHO, limetahadharisha dhidi ya wasiwasi wa kupindukia kuhusu aina mpya ya virusi vya corona vinavyosambaa kwa kasi kubwa, baada ya kugunduliwa nchini Uingereza na baadae Afrika Kusini.

Shirika hilo limesema ni kawaida ya virusi kufanya hivyo. Aina hiyo ya virusi imezua taharuki kote ulimwenguni, hali iliyopelekea mataifa kadhaa kuweka vizuizi vya usafiri kwa Uingereza na Afrika Kusini.

Maofisa wa WHO walisema hawana ushahidi wowote unaoonesha kwamba aina hiyo mpya ya virusi inawafanya watu kuwa wagonjwa zaidi au kuwa ni mbaya zaidi kuliko virusi vilivyokuwepo awali vya ugonjwa wa COVID-19.

Ingawa ilithibitisha kwamba aina hiyo mpya inaonekana kuenea kwa kasi zaidi.