NA FATMA KASSIM

WIZARA ya Afya Ustawi wa Jamii ,Jinsia na Watoto kupitia Kitengo cha Afya ya Mazingira kinakusudia kufanya mashindano ya usafi katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba.

Mashindano hayo yatahusisha kwenye ngazi za halmashauri na Manispaa na shehia na lengo kubwa la mashindano hayo ni kushajihisha jamii katika masuala mazima ya usafi na kuepukana na maradhi ya Miripuko ikiwemo kipindupindu.

Hayo yameelezwa na ofisa Afya Kitengo cha Afya ya Mazingira, Forogo Kibwana Mtande katika mkutano wa wasimamizi wa mashindano ya usafi ambapo mashindano hayo yatafanyika mwanzoni mwa mwezi wa Januari.

Alisema wamepanga kufanya mashindano hayo kutokana na kuwa bado hali ya usafi katika maeneo mbali mbali hairidhishi na mashindano hayo yatasaidia kuweka miji kuwa katika hali ya usafi.

Alifahamisha mpango huo utasaidia kushajihisha Mabaraza ya miji katika kutengeneza mpango mzima wa kusimamia masuala ya usafi ili kuweza kutomeza maradhi ya kuambukiza.

Alisema mashindano hayo yatalenga maeneo mbali mbali yakiwemo masoko, maskuli vituo vya mazingira kwa ujumla na watapita kuangalia usafi katika sehemu hizo.

Naye ofisa Afya Mazingira kutoka Tanzania bara, Honest Anicetus alisema kwa upande wao mpango huo umewasaidia sana katika kuimarisha masuala ya usafi katika miji mbali mbali.

Alifahamisha lengo la mashindano ya usafi wa mazingira ni kutoa changamoto na kuhamasisha manispaa, mabaraza ya miji na wilaya, wadau na jamii kwa ujumla kuzingatia umuhimu wa kuinua kiwango cha afya na usafi wa mazingira ili kuzuia na kupunguza kasi ya kuenea kwa magonjwa yanayotokana na uchafu.

Aidha alisema mashindano hayo ya afya na usafi wa mazingira yanalenga kufanikisha mambo mbali mbali yakiwemo kuhamasisha uandaaji wa mipango na utekelezaji endelevu wa shughuli za afya pamoja na kuongeza uwajibikaji kwa watendaji na wadau katika suala zima la usafi wa mazingira.

Nao washiriki wa mkutano huo walisema kuwa walisema kuwa watahakikisha wanasimamia vyema mpango huo ambao utakuwa endelevu katika kuimarisha usafi wa afya ya mazingira.

Walisema ili kuhakikisha maeneo yote yanashiriki kikamilifu katika mashindano hayo, ushindanishi utafanyika katika hatua mbili ambapo hatua ya kwanza itahusu mashindano.