NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM
MAKAMU Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Frederick Mwakalebela, ameanza kulipigia hesabu kombe la Mapinduzi cup.


Michuano hiyo ya Mapinduiz inatarajiwa kuanza mapema mwakani.


Timu ambazo zitashiriki kwenye michuano hiyo kutoka Tanzania Bara ni, Simba SC, Yanga SC, Azam FC, Namungo FC na bingwa mtetezi ambaye ni Mtibwa Sugar.


Akizungumza na Zanizibar Leo jana kwa njia ya simu, Mwakalebela alisema anaimani watashiriki kwenye michuano hiyo na lengo lao ni ubingwa.


Alisema watashiriki mapinduzi cup kwa lengo la kuhakikisha wanatwaa ubingwa kwani watapeleka kikosi kamili.