NA MWANDISHI WETU

KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Cedric Kaze kimeendeleza rekodi ya kucheza mechi zake za Ligi Kuu Bara bila kupoteza baada ya kushinda mabao 3-0 dhidi ya Ifefu.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Deus Kaseke dakika ya 13. Bao hilo lilidumu mpaka muda wa mapumziko na kuwafanya Ihefu kwenda kwenye mapumziko wakiwa nyuma kwa bao moja.

Kipindi cha pili Yanga ndani ya Uwanja wa Sokoine iliongeza bao la pili dakika ya 50 kupitia kwa Yacouba Songne na bao la tatu na la mwisho lilifungwa na Feisal Salum dakika ya 60.

Msumari wa mwisho uliopigwa na Feisal unafanya Yanga ifunge jumla ya mabao 28 katika mechi 17 za Ligi Kuu Bara.

Ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 43 huku nyota wao mpya Saido Ntibanzokiza akizidi kuonyesha makeke ndani ya uwanja.