NA TIMA SALEHE,DAR ES SALAAM

KIKOSI cha Yanga, kinatarajia kuendeleza ubabe wake dhidi ya maafande wa Tanzania Prisons mchezo katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara.

Mchezo huo utachezwa kwenye dimba la Nelson Mandela, Mkoani Sumbawanga.

Mchezo wao uliopita wananjangwani hao walipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ihefu FC.

Akizungumza na Zanzibar Leo jana , Ofisa mhamasishaji wa klabu hiyo Antonio Nugaz, alisema kwamba timu yao inaenda kuendeleza pale ilipo ishia.

Alisema mpira ni dakika 90 na wanaimani watazitumia vizuri kuhakikishia wanapata ushindi na kuendelea kusalia kileleni mwa msimamo.

Mchezo mwingine ambao utachezwa siku hiyo ni Polisi Tanzania dhidi ya Azam FC kwenye uwanja wa Ushirika mkoani Kilimanjaro.