NA ZAINAB ATUPAE

JUMUIYA ya ZANVARSITY ALUMNI ambayo inamiliki timu ya mpira wa miguu imefanya uchaguzi wa jumuiya hiyo watakaokuwa madarakani kwa miaka mitatu.

Uchaguzi huo ulifanyika katika ukumbi wa hoteli ya Bangalow Paradise iliopo Pwani Mchangani, ambapo wajumbe 45 walipiga kura.

Akitangaza matokeo hayo mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, Said Soud Abdalla, alitaja mshindi nafasi ya Mwenyekiti ni Shaban Ramadhan Shaban kura 39.

Nafasi ya makamu mwenyekiti ilichukuliwa na Ameir Mohamed Makame kwa kura 36, nafasi ya katibu ilikwenda kwa Taki Abdalla Taki aliyejikusanyia kura 40.

Naibu Katibu ni Slim Said Abdalla aliyepata kura 45,huku nafasi ya mshika fedha ikichukuliwa na Dk. Othman Abbas kura 41.Naibu Mshika Fedha ni Abubakar Mohamed Abuubakar ambaye alipata kura 43.

Wajumbe Nasim Faki Mfaume,Jambia Said Jambia,Mustafa Abdulhamid Haji na Dk. Abdalla Issa wote hao walipata kura 45.

Akizungumza mara kumaliza uchaguzi huo mwenyekiti wa Shaban Ramadhan Shaban,alisema Jumuiya ina malengo mengi ikiwemo kusaidia jamii za watu wasio jiweza.