NA AMEIR KHALID, DAR ES SALAAM,

TIMU ya Ndijani ya mchezo wa ‘Softball’ imefanya vyema katika mshindano ya taifa ya mchezo huo baada ya kushinda michezo yake.

Ndijani ilishuka dimbani jana katika viwanja vya skuli ya Azania a Dar es Salaam katika mchezo uliopigwa saa 2:00 asubuhi, Ndijani ilishinda kwa pointi 14 – 4 dhidi ya Kibamba.

Aidha katika mchezo huo wanadada wa Ndijani walianza kwa nguvu na kuwatia hofu wapinzani wao ambao hadi raundi ya kwanza inamalizika Ndijani iliongoza kwa pointi 8 – 2.

Kuingia mzunguruko wa pili Ndijani iliwadhibiti wapinzani wao na kufanikuwa kuvuna pointi nyengine na kufikisha udadi ya pionti 14 – 4.

Mchezo wa pili ulipigwa majira ya saa 8:00 mchana ambapo Ndijani iliwashinda kirahisi timu ya Kibwegele kwa kuwafunga pointi 19 – 9.

Baada mchezo huo mkuu wa msafara wa timu za Zanzibar Khatib Mohammed Khatibu, amewapongeza wachezaji kwa ushindi walioupata na kuwataka kuendelea na juhudi katika michezi iliyobaki.

Aidha alisema licha ya hali ya hewa ya joto kali katika mkoa wa Dar es Salaam, vijana wamecheza kwa nguvu na ari kubwa mpaka kushinda michezo hiyo.

Pia aliwaomba Wazanzibari kuendelea kuwaombea dua ili kutimiza ndoto za ushindi walizojiwekea.