NA MWAJUMA JUMA
TIMU ya soka ya Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) imeanza kwa sare katika michezo yake ya kirafiki waliocheza Dodoma.


Timu hiyo ambayo ipo Mkoani huko kwa ziara ya kimichezo ilishuka dimbani juzi kucheza na Kahawa SC kutoka Unguja na kutoka sare ya kufungana mabao 2-2.


Katika mchezo huo ambao ulichezwa kwenye kiwanja cha skuli ya sekondari ya Dodoma miamba hiyo ambayo yote ipo kwa lengo moja iliweza kucheza mechi ya ushindani iliyotowa burudani tosha machoni mwa mashabiki.


ZECO katika mchezo huo mabao yake yalifungwa na Ali Nassor Mohammed kwa mkwaju wa penalit dakika ya 49 baada ya mchezaji wao Mohammed Ali Ramadhan kuangushwa na la pili lilifungwa na Mussa Ali Hassan dakika ya 83.


Kwa upande wa timu ya Kahawa sports club mabao yao yamefungwa na Abdalla Ali kidula dakika ya 59 na bao la pili limefungwa na Abdalla Juma Abdalla Dakika ya 62.