NA ZAINAB ATUPAE

TIMU ya  soka ya Uchapaji imefanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mdhibiti ikiwa ni muendelezo wa mashindano ya Mawizara,Mashirika  na Taasisi za Serikali.

Mtanange huo uliotimua vumbi majira ya saa 2:00 asubuhi uwanja wa Mao Zedong.

Mchezo huo ulikuwa wa ushindani,huku kila timu ikitafuta ushindi kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa mashinano hayo.

Hadi timu zinakwenda mapumzikoni Uchapaji ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-1.

Mdhibiti ndio ilikuwa ya kwanza kuzifumua vyavu za wapizani wao dakika ya nne kupitia  Sabri Abeid,huku mabao mawili ya Uchapaji yaliwekwa wavuni na Haji Hassan Mdungi dakika ya tisa na dakika ya 21.