NA VICTORIA GODFREY

KOCHA Mkuu wa timu ya mpira wa Wavu JKT Papaa Khamis Papaa amesema siri ya mafanikio ya ushindi ni maandalizi mazuri walioyafanya.

JKT wanaume na Wanawake wameibuka na ushindi baada ya kuwafunga wapinzani wao kwenye michezo ya fainali ya mashindano ya Wavu Kombe la Mapinduzi ya Zanzibar yaliyomalizika juzi .

JKT wanaume iliibuka na ushindi huo baada ya kuifunga Nyuki seti 3-0 katika mchezo uliochezwa Jumatatu,wakati Wanawake JKT waling’ara baada ya kuwaadhibu Mkalapa Girls seti 3-0 .

Akizungumza na gazeti hili Papa,alisema mashindano yalikuwa magumu ,kwani timu zote zilijipanga kufanya vizuri ili kuchukua ubingwa.