NA VICTORIA GODFREY

UONGOZI wa Kamati ya Paralimpimki Tanzania (TPC) umesema mwisho wa kuchukua fomu za kuomba uongozi Januari 15 mwaka huu.

Uchaguzi wa TPC umepangwa kufanyika Januari 23 ambapo viongozi mbali mbali watachaguliwa.

Katibu Mkuu wa TPC, Tuma Dandi ,alisema milango bado ipo wazi kwa watu wenye nia ya kuomba nafasi ya uongozi.

Alisema hadi sasa kuna mwitikio mzuri wa idadi ya wagombea wanajitokeza kuchukua fomu.

” Mwitikio ni mzuri wa watu wanajitokeza,hivyo tunasubiri tarehe ya mwisho ndio tutajua idadi ya watia nia na tutaweka hadharani na uchaguzi upo palepale,” alisema Dandi