NA MWANAJUMA MMANGA

JESHI la polisi Mkoa wa Kusini Unguja linamshikilia kijana Abdul Suleiman Abdull (29) mkaazi wa Bwejuu kwa kosa la kupatikana na nyongo tano za bangi zinazoaminika kuwa ni dawa za kulevya.

Akithibitisha kukamatwa kwa kijana huyo Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Suleiman Hassan Suleiman, alisema tukio hilo limetokea Disemba 3:30 usiku huko Paje kwa Komando Wilayani humo.

“Juhudi za kumpata kijana huyu zilifanikiwa baada ya jeshi hili lilikuwa likifanya opereshini maalum ya kuwasaka wahalifu, watumiaji na wasambazaji wa dawa za kulevya katika maeneo ya mkoa huo” alisema Kamanda Suleiman.

Alisema kijana huyo, alipatikana na nyongo hizo ambazo alizokuwa amezihifadhi ndani ya plastiki ya sigara aina ya Sporngmen ambayo alikuwa nayo mkononi wa kulia akijua kuwa ni kosa la kisheria na mtuhumiwa huyo yuko chini ya ulinzi wa jeshi la polisi kwa ajili ya upelelezi zaidi. 

Kamanda Suleiman alisema wamekuwa wakifanya operesheni za mara kwa mara za matukio kama hayo ili kukomersha vitendo kama hivyo.