KWA hakika makundi ya kigaidi yanajitahidi sana kuwavuta vijana wajiunge nao na kutekeleza mikakati mibaya kwa njia mbali mbali na kwa kutumia mbinu nyingi ama kwa kuwashawishi kwa pesa, safari, madaraka nakadhalika.

Jihad ambayo ilifaradhishwa ili kuinusuru dini na kuwasaidia waislamu wenzao. Pia, makundi haya yanafuata njia za kuchafua mawazo na kubadilisha itikadi na uelewa yakitumia mbinu nyingi za kuwadanganya vijana hawa na kuwashawishi.

Ili tuweze kupambana na vita ya kimawazo hiyo na kukabiliana na hali hiyo ya kuwavuta vijana ambao ndio silaha iliyo muhimu zaidi kujenga na kuendeleza jamii, nchi na dunia nzima.

Katika makala haya tutazungumzia baadhi ya mbinu za makundi ya kigaidi kuwavuta na kuwakinaisha vijana wakubali mawazo ya makundi haya na kufuata njia za kumwaga damu na kuharibu jamii na kupoteza amani na utulivu, tukitilia mkazo mbinu za kundi la Daesh (ISIS) ambapo mbinu za kundi hili zilifuatwa na makundi mengine kama vile; Al-Shabab, Boko Haram, Taliban, Al-Qaidah nakadhalika.

Tamko la “Daesh” limekuwa linasemwa sana katika vyombo vya habari sawa vinavyoandikwa, vinavyotazamiwa au vinavyosikilizwa, tamko hilo likawa linaashiria picha za umwagaji damu, kuwachoma wanadamu na kufanya uharibifu kwa jina la dini!

Kundi hilo la kigaidi halikutosheleza kwa kufanya jinai kubwa dhidi ya wanadamu na staarabu za kibinadamu, bali linafanya juhudi kubwa kwa ajili ya kueneza mawazo yake machafu na yasiyo sawa kwa lugha tofauti likitumia mapinduzi na maendeleo ya kiteknolojia katika uwanja wa mawasiliano ya kijamii ili liweze kuwavutia vijana wa kiislamu kutoka pande zote duniani wajiunge nalo. Basi ikawa ni wajibu juu ya Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar Al-Shareif kufuatilia kwa makini kila yaliyotangazwa na kundi hilo na kuyachunguza ili kuwasaidia vijana wa kiislamu wajiepushe na kutoathirika na misimamo mikali na vurugu ya kundi hilo.

Watafiti wa kituo wamechunguza matoleo ya “Daesh”, wameainisha nguzo maalumu za udanganyifu ambazo kundi hilo linazitegemea katika yaliyotangazwa nalo, nguzo hizo na kama yafuatayo:
Kutegemea na kutotaja maelezo ya kifiqhi yanayosababisha kuhitalifiana na ambayo yanaweza kuwafanya walengwa wasikie uchoshi hasa wasio na mafunzo ya kutosha kuhusu maudhui ya suala linalojadiliwa.

Kudhihirisha kwamba maoni yao ni ya kweli yasiyo na shaka, ambapo tunawakuta wanataja katika maandishi yao matamshi kama vile: “wanavyuoni wa fiqhi wamekubaliana juu ya ….”, “maulamaa wote wameambatana juu ya ….”.
Mambo mengine ni kutegemea matini na hadithi ambazo zinaunga mkono wazo lao bila ya kuangalia matini zinazozipinga matini hizo, ilhali inapaswa kuangalia matini za pande mbili kwa ajili ya kubainisha wazo na kuondoa utata, isitoshe, bali zaidi ya hayo kwa kuziambatanisha matini tofauti hizo na kuzifahamu tutatambua kwamba dalili zitakuwa hoja za uharibifu wa fikira zao sio kuziimarisha.

Aidha kuchukua sehemu na kuacha sehemu kutoka matini kutokana na matakwa na maadili yao.

Sambamba na hilo, lakini kutofahamu kwao zile matini wanazozitaja kwa sababu ya uchache wa elimu yao katika uwanja wa taratibu za lugha na kutotambua kwao kanuni za sheria na kutofahamu kwao maana za matamshi yaliyotajwa katika vitabu vya vyanzo vya fiqhi (Usuul Al-Fiqh).

Kuwa na maana ya pamoja, kuwa na maana karibu, kuwa na maana sawa, kuwa na maana iliyofichika na kuwa na maana hasa, na kutotambua kwao maana ya yanayotamkwa na yanayofahamiwa na tofauti baina ya yanayofahamiwa kwa mwafaka na yanayofahamiwa kwa tofauti na kutomakinisha kwao kutambua tofauti iliyopo baina ya madhumuni ya maudhui na umbo lake.


Matini wanayoichukua kama ni dalili pengine huwa matini ya kijumla ambayo maelezo yake yamekuja katika sehemu nyingine kwenye Qurani au Sunnah au Ijmaa au Qiyaas, lakini hawajui cho chote kuhusu sababu za kujumlisha kama vile; kuwa na maana za pamoja, kuweka mbele au kuchelewesha, kuficha maana na kadhalika kati ya yaliyopitishwa na wanavyuoni wa Usuul vitabuni mwao.

Sambamba na hilo, lakini Kutotambua kwao kabisa la kijumla na ya hasa hasa na tofauti baina ya la kijumla linalokusudiwa na la kijumla linalokusudiwa kwake kuhusisha.

Aidha kutoelewa kwao kabisa kwa lisilo na masharti na lenye masharti na vidhibiti na lini inapaswa kufanya lisilo na masharti sawa na  lenye masharti na lini inapaswa kuacha kila moja katika hali ile ile?

Kutegemea hotuba za hisia ambazo zinachemsha hisia za kidini za wanaoihofia dini yao jambo linalowadhihirisha kwa maoni ya wale – waliodanganywa na hotuba zao kwamba wao ndio waislamu wa kweli wanaojilazimisha na dini ya Mwenyezi Mungu katika ardhi yake.

Kutaja matukio ya kihistoria ambayo yanadhihirisha mafanikio ya waislamu na kuyaunganisha na dhana za (uhamiaji) Hijra na (kupigania vita) Jihad na kwamba waislamu hawataweza kupata ushindi na utukufu ila kwa njia ya Jihad na kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa maoni yao finyu na ufahamu wao usio sahihi.

Kuonyesha kwamba mpiganaji “Mujahid” ni mtu mbingwa asiyepatwe na kushindwa kamwe, na kutegemea mbinu za vyombo vya habari vya kisasa kubainisha hivyo pasipo na kuainisha dhana ya Mujahid katika sheria? Na nini maana ya jihad na masharti na vidhibiti vyake? Na nin roli ya mtawala kuhusu jambo hilo?

Kuwadharau waislamu wenye misimamo mikali katika nchi zao na baadhi ya alama za kuwadharau waislamu wa kawaida katika nchi zisizo za kiislamu na kutoa wito wa kuhamia kwa “Daesh” ili kufanya ibada ya dini ya kweli – kwa maoni yao – pasipo na udharau wo wote.

Aidha jambo jengine ni kuwavutia watu kwa kisingizio cha ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa anayepigania njia ya Mwenyezi Mungu akauawa kwamba ataingia peponi na kupata anasa kwa milele, kwa kuzingatia hiyo ni njia mojawapo za kuwadanganya wasiotambua msingi wa dini.

Kugawanyika kwa hotuba zao katika mafungu mawili: la kwanza inaweza kuitwa “mtazamo wa kimafundisho wa Daesh” ambalo linasema misemo na kuijadili kwa haraka na kutaja dalili za kuthibitisha kwamba madai ya Daesh ni ya kweli na yaliyo kinyume chake ni batili, na aina hiyo inawahutubia wanaojua maelezo machache kuhusu masomo au utamaduni wa kati kati au ufahamu wa kidini na fiqhi finyu ambapo watu hao huwa na baadhi ya matatizo kuhusu misimamo mikali ya Daesh kati ya mauaji na machinjo.

Basi kwa kutumia aina hiyo ya hotuba potofu inayoimarishwa na matini zisizo kamili na zilizochukuliwa mbali na mazingira yake, hotuba ya Daesh inaweza kumaliza na kuyatatua matatizo madogo ya wale wanaoyapinga mawazo ya Daesh ili waweze kujiunga na kundi hilo na kujikinaisha kwamba watu hao ni waja wa kweli wa Mwenyezi Mungu wanaoweza kutetea haki duniani.

Ama aina ya pili ya hotuba inaweza kuitwa “hotuba ya kawaida inayotumia hisia” nayo ile hotuba inayowalengea wenye akili finyu wanaosukumwa na hisia zao za kidini lakini wanataka sheria ya Mwenyezi Mungu itawala ulimwenguni, basi hawa huvutwa na maneno na matangazo yanayojinasabisha kwa dini na picha bandia ya mujahid mwenye nguvu isiyo na mfano ambaye anawaua maadui wa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuinusuru dini ya Mwenyezi Mungu.

Kufuta mtazamo wa kuzingatia malengo ya mambo kutoka maoni yao ya kifiqhi yanayohalalisha jinai zao, ambapo mtazamo wa kuzingatia malengo huzifanya kazi zao ni madanganyifu, dhuluma na uadui kabisa yanayotakiwa kuzuiliwa na kuchunguzwa kwa maneno na kupiganiwa kwa vitendo kwa mujibu wa misingi ya kifiqhi.
Aidha kuwahutubia waislamu wasio waarabu kwa njia ya kujumlisha na kutaja matini zisizo kamili kuhusu uwajibu wa uhamiaji kutoka nchi za ukafiri kwenda nchi za Uislamu, na istilahi hizo zikiwa hazina faida kwa mwislamu mwaarabu anayeishi katika nchi inayoruhusu kufanya ibada za kidini, lakini hali kwa mwislamu anayeishi katika nchi za kimagharibi itakuwa tofauti kwa sababu hana matatizo yo yote kuiita nchi anakoishi ni nchi ya ukafiri basi istilahi kama hizo zitapata nafasi ya kuenea na kutumika hasa akiwa yule mwislamu anateseka na tatizo la kudharauliwa na kutopewa uhuru wa kutosha wa kufanya ibada za kidini.

Kuunganisha baina ya Uislamu na dhana za utii kamili “Al-Walaa” na kutotii kabisa au kujikinga “Al-Baraa” na kutia wasi wasi kuhusu ukweli wa Uislamu wa asiyejilazimika na dhana hizo mbili na masharti zao katika njia ya Mwenyezi Mungu na kulifanya wazo la Al-Walaa na Al-Baraa litegemee mauaji, machinjo, kuchoma na uharibifu kwa ye yote anayepinga kundi hilo.

Kusema ibara kama vile: makafiri asili, wanaoacha dini yao, makhaini (wasaliti), majasusi jambo linalomfanya anayekusudiwa na hotuba yao hasa mwenye akili finyu azoea kutumia ibara hizo na kuzikubali, basi haoni dhiki yo yote kuwazingatia wenyeji wa nchi yake ni makafiri na kwamba jeshi lake ni wasaliti wanaostahiki kupiganiwa vita.

Aidha jambo jengine ni kuwavutia vijana kujiunga na Daesh ni kusikia kwao kwa utambulisho wa kidini chini ya matangazo ya kusimamisha sheria ya Mwenyezi Mungu na kuinusuru haki na kurudisha utukufu wa Uislamu.

Pia kutumia suala la kuipinga Marekani na wanaoiunga mkono ambao ni makhaini wenye kufuata mfumo wa kidemokrasia ambao ni waadui wa Mwenyezi Mungu katika nchi za kiislamu ilhali watu hao wanatekeleza mikakati ya Marekani na wasaliti wake wakipigania vita kwa niaba yao.

Kutia wasi wasi kuhusu ukweli wa hotuba ya kidini inayofuata mbinu ya kiwastani ya wanachuoni wa waislamu na kudai kwamba hadithi za wanyonge “Al-Ghurabaa” kama vile: “hatima nzuri sana kwa Al-Ghurabaa” zinawakusudi wao jambo linalowafanya wao ndio Al-Ghurabaa wanaoinusuru haki na kwamba wasiowaunga mkono ni wafuasi wa batili.

Ili kuona hayo yanaipukika tunapaswa tusiache ujinga na fikira zisizo sawa na mawazo mabaya ambayo yanaweza kuhalalisha kwa baadhi ya watu kufanya dhuluma kwa kudai kwamba dini ya kiislamu ni dini ya kuchochea kuuangamiza ubinadamu na kuimarisha uadui na mizozo baina ya dini na tamaduni tofauti, ilhali dini ya Uislamu inaombea upendo, ushirikiano na kueneza maadili mema.

Bado dini ya kiislamu ni dini nzuri na kwamba kuinasibisha na ugaidi ni kuichafua huku dunia ikielewa kuwa ugaidi sio dini bali ni mtu mwenyewe au kikundi cha watu.

Makala haya imetayarishwa na kituo cha Kiislamu cha Misri Dar- Tanzania.

Imeandikwa na;

Alaa Salah Abdulwahed

Mwalimu Msaidiza wa Kiswahili Chuo Kikuu cha Al-Azhar

Mtafiti katika Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Fikra kali