LONDON, UINGEREZA
SHIRIKA la Kimataifa la Kutetea Haki za Binadamu (Amnesty International) limeitaka Ufaransa kusitisha mauzo ya silaha kwa Lebanon ikisema serikali mjini Beirut inazitumia kufanya ukandamizaji wa maandamano ya amani.
Taarifa ya shirika hilo ilisema, silaha zinazotengezwa Ufaransa ikiwemo za mpira, mabomu ya machozi na virungu, kisha kuuzwa kwa Lebabon zinatumika kwenye ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.
Amnesty ilitaka Ufaransa kusitisha mauzo hayo ya silaha hadi mamlaka za Lebabon zitakapokiri kufanya ukandamizaji, kwa sababu vikosi vyake vya usalama vinafanya kazi bila kuzingatia sheria.
Kulingana na shirika hilo, ushahidi uliyokusanywa unaonesha kuwa, silaha za Ufaransa zilitumika mara kwa mara kwenye maandamano dhidi ya serikali ya mwaka 2015, 2019 pamoja na Agosti mwaka uliopita.