BERLIN,UJERUMANI

KANSELA wa Ujerumani Angela Merkel amewataka wananchi wake waendelee kuwa na nidhamu katika kupambana na janga la maambukizi ya virusi vya corona.

Kansela Merkel alisema hayo katika hotuba ya mwaka mpya.

Merkel alisema katika kipindi cha miaka 15 iliyopita mwaka wa 2020 ulikuwa mgumu kuliko yote mengine kutokana na janga la maambukizi ya virusi vya corona.

Watu milioni 1.7 walikumbwa na virusi hivyo nchi Ujeruamni na zaidi ya 32,000 wameshakufa.

Kiongozi huyo wa Ujerumani alipinga vikali nadharia za uzushi juu ya maradhi hayo na amesifu juhudi za madaktari na wote wanaouhusika na tiba.

Hata hivyo alikiri kuwa maradhi hayo yalileta changamoto isiyokuwa na kifani katika karne hii kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Aidha, katika hotuba yake Kansela Merkel alielezea matumaini juu ya kupambana na maambukizi kutokana na chanjo zilizopatikana.