LONDON, England

MIKEL Arteta,Kocha Mkuu wa Arsenal amesema wachezaji wake wana kazi ya kulinda viwango vyao, ili kuendelea kupata ushindi kwenye mechi zao zote zijazo pamoja na kuongeza hali ya kujiamini.

Arsenal ikiwa Uwanja wa Emirates iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Newcastle United jambo ambalo limemfurahisha Arteta.

Mabao ya Arsenal yalifungwa na nahodha Pierre Emerick Aubameyang ambaye alifunga mawili dakika ya 50 na 77 na bao moja alifunga Bukayo Saka dakika ya 60.

Ushindi huo unaifanya Arsenal kufikisha jumla ya pointi 27 ikiwa nafasi ya 10 baada ya kucheza mechi 19 huku Newcastle ikiwa nafasi ya 15 na pointi 19 baada ya kucheza mechi 18.

Kinara ni Manchester United inayonolewa na Ole Gunner Solskjaer ikiwa na pointi 37 ambaye amesema wachezaji wake walipambana mithili ya kupanda mlima Kilimanjaro.