NA MWANAJUMA MMANGA

MTU mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi Mkoa wa Kusini Unguja kwa kosa la kupatikana na bangi  yenye uzito wa kilogram tano baada ya kupekuliwa mwilini mwake huko kwenye fukwe za Paje, Januari 24 mwaka huu.

Akithibitisha kukamatwa kwa kijana huyo, Kamanda wa Polisi mkoa huo, Suleiman Hassan Suleiman, alimtaja kijana huyo Moses Isaac Mosses (27) mkaazi wa  Jambiani wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Alisema kuwa kijana huyo alikamatwa kufuatia jeshi la polis lilifanya opereshen maalum ya kuwasaka wanaouza unga, wasambazaji, watumiaji na wahalifu katika mkoa huo.

Alisema Kamanda mtuhumiwa huyo ni muuzaji na hivi sasa yuko chini ya jeshi la polisi kwa ajili ya kuendelea na hatua ya upelelezi zaidi na  aliwataka vijana kuacha kujishugulisha na biashara hiyo na badala yake kufanya biashara halali na kujitafutia rizki.

Wakati huohuo, ajali ya gari kugongana na pikipiki na kusababisha majeruhi mnamo Januari 25 mwaka huu majira ya Saa 6:01 huko Kitumba katika Wilaya ya kati mkoa wa Kusini Unguja gari yenye namba za usajili Z 914 AW aina ya Toyota Carina ikiendeshwa  na Haji Omar Iddi (24) mkaazi wa Mangapwani.

Alisema kijana huyo alikuwa  akitokea Kwambani kuelekea Kidimni aligongana na pikipiki yenye namba za usajili Z.841 aina ya Saund ikiendeshwa na Omar Abdalla Rajab (18) mkaazi wa Machui kuelekea Kitumba akiwa amewapakia Lela Lela Petrol Magudi (32)mkaazi wa Bububu ana Fatma Abadalla (28)mkaazi wa Bububu.

Kamanda Suleiman, alisema katika ajali hiyo lela amepata majeraha sehemu ya usoni na mguu wa kulia na Fatma amepata majeraha kichwani na mguu wa kushoto wote wamelazwa hospitali ya Mnazi mmoja na wanaendelea vizuri.

 Alisema chaqnzo cha ajali hiyo ni kushindwa kusimama kwa dereva wa pikipiki kwenye makutano ya barabara na  aliwataka wadereva kuwa waangalifu pale wanapokuwa njiani ili kuepusha jail zisizokuwa za ulazima.