NA TATU MAKAME

KIJANA aliyetenda makosa sita kwa wakati mmoja kwa kumbaka na kumtorosha msichana aliye chini ya uangalizi wa wazazi, anatarajiwa kupandishwa mahakamani Januari 11 mwaka huu.

Kijana huyo aliyefahamika kwa jina la Ame Omar Ramadhani (27) mkaazi wa Dimani Branji Wilaya ya Magharibi ‘B‘ Unguja, anatarajiwa kupandishwa tena mahakama ya Mkoa Vuga kuendelea na kesi hiyo.

Mshitakiwa huyo ambae yuko rumande baada ya kukosa dhamana kutokana na kesi yake kuwa haina dhamana, alisomewa makosa yake na Mwendesha Mashitaka, kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Asma Juma, mbele ya Hakimu Makame Mshamba Simgeni.

Alisema mshitakiwa huyo alitenda makosa sita kwa nyakati tofauti.

Awali akisoma makosa hayo, Mwendesha Mashitaka huyo alisema, kosa la kwanza ni kumtorosha mtoto aliye chini ya uangalizi wa wazazi wake mwenye umri wa miaka 16, jambo ambalo ni kosa kisheria kwa mujibu wa kifungu cha 113 (1) (b) cha sheria namba 6 ya mwaka 2018 sheria za Zanzibar.

Ilidaiwa kuwa, mnamo Agosti 7 mwaka 2019 majira ya saa 7:00 mchana, mshitakiwa huyo alimtorosha msichana aliye chini ya uangalizi wa wazazi wake kutoka Dimani Branji na kumpeleka nyuma ya skuli ya Msingi Dimani, kitendo ambacho ni kosa kisheria.

Kosa la pili ni siku ya Agusti 8 mwaka 2019, mshitakiwa huyo alimbaka msichana huyo jambo ambalo ni kosa kisheria.

Ilidaiwa kuwa siku hiyo, mshitakiwa huyo majira ya saa 10:30 asubuhi alimtorosha msichana huyo bila ya ruhusa ya wazazi wake na kumpeleka nyuma ya skuli ya msingi ya Dimani kitendo ambacho ni kosa.

Kosa la tatu ni kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 16 ambae yupo chini ya uangalizi wa wazazi wake, jambo ambalo ni kosa kisheria.

Ilidaiwa kuwa mnamo Agosti 8 mwaka 2019, mshitakiwa huyo alimbaka msichana aliye chini ya uangalizi wa wazazi wake.

Kosa la nne ni mnamo Agosti 2019 majira ya saa 12:45 mchana, alimbaka tena msichana huyo jambo ambalo ni kosa kisheria.

 Kosa la tano mnamo Agosti 17 mwaka 2019, alimtorosha msichana aliye chini ya uangalizi wa wazazi wake mnamo majira ya saa 8:00 mchana, kwa kumtoa nyumbani kwao na kumpeleka msituni nyuma ya skuli ya maandalizi Dimani.

Kosa la sita ni kumbaka msichana huyo kitendo ambacho ni kosa kisheria.

Ilidaiwa kuwa mnamo Mei 17, 2019, majira ya saa 6:00 mchana alimuingilia msichana huyo jambo ambalo ni kosa kisheria.

Hata hivyo mshitakiwa huyo hakupewa dhamana na yuko rumande hadi Junuari 11 mwaka huu kesi yake itakaposikilizwa.