NA MWAJUMA JUMA
TIMU ya soka ya Kombaini ya Zanzibar imeshindwa kutamba mbele ya Azam FC kwa kukubali kichapo cha mabao 2-1, katika mchezo wa kirafiki uliochezwa juzi usiku uwanja wa Amaan.
Miamba hiyo ambayo ilishuka dimbani hapo majira ya saa 2:00 za usiku ambapo ambao ulikuwa mzuri.
Zanzibar ambayo ilikuwa chini ya kocha Ali Suleiman Mtuli licha ya kutangulia kupata bao, lakini walijikuta wakiridhika na matokeo hayo na kusawazishiwa na kwenda mapumziko wakiwa sare ya kufungana bao 1-1.
Katika mchezo huo ambao ni maalumu kwa ajili ya Azam kuendelea kupata mazoezi ya kujiandaa na ligi kuu ya Tanzania Bara, Azam tayari imeshashuka dimbani mara tatu ambapo kati ya michezo hiyo imeshinda michezo miwili na kufungwa mmoja.
Mabao ya washindi hao yaliwekwa kimiyani na wafungaji wake Iddi Suleiman na Prince Dube wakati la Zanzibar lilifungwa na Mundhir Abdalla Vuai