NA TATU MAKAME

JESHI la Polisi MKoa wa Kaskazini Unguja, limesema litaendelea na operesheni zake za kupambana na watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya kwani tatizo hilo limekuwa likiathiri vijana walio na umri mdogo pamoja na kupoteza nguvu kazi ya taifa.

Akizungumza na Zanzibarleo,Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Haji Abdalla Haji alisema kuwa mapambano hayo yataendelea katika maeneo yote ya mkoa.

Alieleza kuwa licha ya juhudi zinazochukuliwa, lakini bado kuna watu wanaoendelea na biashara hiyo haramu ambayo inapaswa kupigwa vita a kila mwananchi.

Kamanda huyo, alisema Januari 1, mwaka huu majira ya saa 5:20 asubuhi walimkamata Catherine Ibrahim Massam (28) mkaazi wa Nungwi Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja, akiwa na bangi      yenye uzito wa grams 400 ambayo aliihifadhi katika chumba chake anachoishi.

Alifahamishwa kwamba mafurushi hayo mawili ya bangi moja likiwa ndani ya mfuko wa plastiki rangi  nyeusi wenye kuonyesha kisha kuhifadhiwa ndani ya mfuko wa kaki na baadae kuwekwa kwenye kidoo  cha rangi ya maziwa.

Hata hivyo, alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara taratibu zitakapokamilika na sasa yuko chini ya ulinzi wa jeshi la polisi.