ZASPOTI
BARCELONA wanatarajiwa kumkosa mchezaji wanayemlenga katika dirisha la uhamisho la Januari, na wagombea urais wa klabu wakiamua kusubiri hadi Juni wakati mlinzi huyo wa Manchester City, Eric Garcia atakapokuwa huru.
Wakatalunya hao wamepata mafunzo kwa Garcia, ambaye mpango wake unaelekea tamati ManCity na hajaficha siri ya azma yake ya kuhamia Camp Nou.


Ilielezwa mapema wiki hii kwamba Barca na Garcia walikuwa wamekubaliana masharti ya kibinafsi, lakini, kazi bado inahitajika kufanywa kuishawishi ManCity kumuuza mnamo Januari.
Joan Laporta anapewa nafasi ya kutajwa kama rais mpya wa klabu, na anataka hakuna maamuzi makubwa ya kifedha kufanywa hadi rais mpya achaguliwe.


Laporta anahisi itakuwa busara kwa klabu kusubiri hadi majira ya joto na kumchukua mchezaji huyo kwa uhamisho wa bure.
“Ikiwa uhamisho utafanywa sasa tutalazimika kulipa ada ya uhamisho pamoja na mshahara wa mchezaji.”
Uchaguzi wa urais wa Barcelona ulipangwa kufanyika Januari 24, lakini, klabu imethibitisha kuwa umeahirishwa kwa sababu ya janga la ‘corona’.(Goal).