NA NASRA MANZI

TIMU ya Baraza la Wawakilishi imefanikiwa kuibuka na ushindi baada ya kuifunga NMB bao 1-0.

Mchezo huo wa kirafiki kwa ajili ya kusherekea mapinduzi ya Zanzibar,uliopigwa majira ya saa 10:00 jioni kwenye uwanja wa Amaan.

Pambano hilo lilikuwa na ushindani na kuhudhuriwa na mashabiki kiasi.

Mnamo dakika ya 33 timu ya Baraza la wawakilishi ilipata bao hilo pekee lililofungwa na Abdulswamad Abdalla Ali.

NMB imefanya mabadiliko ambapo ilimtoa  Martin Masawe na kumuingiza Hesborn Mpate.

Wakati Baraza la Wawakilishi ilimuingiza Daudi Hamadi na kumtoa  Mihayo Juma Nhunga.

Mgeni rasmi katika mchezo huo alikuwa Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, na timu zilipatiwa zawadi za medali.