MCHEZAJI wa zamani wa Uholanzi, George Boateng, amesema, ana lengo la kuwa kocha wa timu ya taifa ya Ghana siku zijazo.

 Boateng aliyezaliwa Ghana katika mji wa Nkawkaw, amesema, hana nia ya kumharibia kazi kocha wa sasa wa CK Akonnor.

 Kiungo huyo mstaafu alihamia Uholanzi akiwa mtoto ambapo alikuwa akiiwakilisha timu ya taifa hilo, katika ngazi za kimataifa, aliwahi kukipiga na Aston Villa, Hull City, Coventry City na Middlesbrough katika Ligi Kuu ya England.

Boateng kwa kwa sasa ni kocha mkuu wa timu ya Aston Villa chini ya umri wa miaka 23.