ACCRA, Ghana
MCHEZAJI wa zamani wa Uholanzi, George Boateng, amesema, ana lengo la kuwa meneja wa timu ya taifa ya Ghana siku zijazo.
Boateng aliyezaliwa Ghana katika mji wa Nkawkaw, amesema, hana nia ya kumuharibia kazi kocha wa sasa wa CK Akonnor.


Kiungo huyo mstaafu alihamia Uholanzi akiwa mtoto ambapo alikuwa akiiwakilisha timu ya taifa hilo katika ngazi za kimataifa, aliwahi kukipiga na Aston Villa, Hull City, Coventry City na Middlesbrough katika Ligi Kuu ya England.


Akizungumzia kuhusu ndoto zake za kuifundisha ‘Black stars’, alisema: “Ikiwa Black Stars wananihitaji, siku zote nitakuwa nipo tayari”, alisema, Boateng.
“Siku zote nimekuwa nikisema nipo kwa ajili ya kusaidia, nina uhusiano mzuri na GFA, (rais Okraku, makamu wa rais, Mark Addo na wanafanya kazi nzuri hivi sasa”.


Aidha, Boateng, alisema: “Siku zote nimekuwa nikionesha kwamba nipo tayari kutoa msaada wangu, kama tutakuwa pamoja tukaweka mawazo yetu sehemu moja na kukubaliana, litakuwa ni jambo kubwa”.
Boateng (45), alianza kuifundisha Kelantan ya Malaysia mwaka 2014 kabla ya kujiuzulu na Blackburn Rovers mwaka 2013 ambapo kwa sasa ni kocha mkuu wa timu ya Aston Villa chini ya umri wa miaka 23.(Goal).