HATIMAYE wabunge nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wametimiza azma yao ya kumuondoa madarakani waziri mkuu wa nchi hiyo Sylvestre Ilunga Ilukamba.

Katika zoezi hilo Ilukamba hakuwepo wakati wa kura ya kutokuwa na imani naye iliyopigwa bungeni, ambapo baada ya kupigwa kura hiyo amepewa saa 24 kujiuzulu kwenye nafasi hiyo.

Wabunge wanamshutumu Ilukamba kwa ushirika wake na rais wa zamani wa nchi hiyo Joseph Kabila, sambamba na hili shutuma nyengine dhidi yake ni serikali yake imejaa mawaziri wabovu.

Kuanguka kwa serikali kunafungua milango kwa rais wa nchi hiyo Félix Tshisekedi kuteua mawaziri mkuu mpya ambaye atakuwa mtiifu kwake na sio kwa utawala uliopita.

Itakumbukwa kuwa mwezi uliopita, rais Tshisekedi aliuvunja muungano ulioundwa na mtangulizi wake, ambapo katika serika hilyo mawaziri wengi walikuwa washirika wa utawala uliopita unaomuunga mkono Joseph Kabila.

Tangu wakati huo, Tshisekedi amekuwa akiwashawishi wabunge kuachana na muungano wa Kabila, ambao hapo awali ulishikilia wengi bungeni, ukikwamisha mpango wa rais wa mageuzi.

Hii itakuwa ni kwa mara ya kwanza nchini DRC katika historia ya miaka 60, serikali ikilazimishwa kujiuzulu kwa kupigiwa kura ya kutokuwa na iamani bungeni.

Kwa sasa rais wa Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo, Félix Tshisekedi, aliamua kuweka mpango wa kuivunja serikali ya muungano ambayo inawashirikisha wafuasi wengi wa aliyekuwa rais wa taifa hilo, Joseph Kabila.

Rais Tshiseked alisema alipata ushauri wa wiki tatu kabla ya kutoa tangazo hilo la kusitisha serikali ya muungano na chama kinachoongozwa na Kabila.

Tshisekedi alisema alishindwa kutekeleza mahitaji ya Wacongo kwa kipindi cha miaka miwili kutokana na changamoto ya serikali ya muungano ambayo ilikuwa ikikwamisha mipango yake.

Hivyo jambo muhimu ambalo ameliafikia ni kuchagua maofisa wapya kuunda baraza jipya kwani bunge la sasa lina wafuasi wengi wa Kabila ambao hawamsikilizi na wala hawana utiifu.

Hapo awali rais Tshiseked alipanga amejiandaa kuvunja bunge lote kama kuna ulazima. “Ni wakati muafaka wa kuzingatia maadili, kanuni na mfumo wa mipango iliyopo. Hivyo ni muhimu kufanya mageuzi yakinifu na sahihi katika bunge lililopo sasa ni muhimu”, alisema Tshiskekedi.

”Kwasababu hiyo, nimeamua kumteua ‘mtoa taarifa’, kwa mujibu wa katiba kifungu namba 78, aya ya pili.” aliongeza

Mtoa taarifa huyo atawajibika kuainisha watu watakaokuwepo kwenye serikali mpya ya muungano, ambayo itakuwa na wajumbe wengi ambao ni wafuasi wa chama kilichopo madarakani tofauti na awali.

Kwa mujbu wa rais Tshisekedi, utakuwa muungano mpya ambao serikali utauweka na kufanya kazi kwa miaka iliyosalia ya uongozi wake.

Kwa maono yake ili kufanikisha kukidhi matakwa ya watu mabadiliko hayo yanapaswa kufanyika.

Kwa maana nyingine, sababu ya kusitisha muungano huu ni kukabiliana na mvutano uliopo ambao unaweka kizuizi katika jitihada za serikali.

Takribani miaka miwili sasa, DRC iliunda serikali ya muungano, baina ya chama cha kabila na chama cha rais mpya Tshisekedi, vyama viwili ambavyo vilipingana kwa kipindi cha muda mrefu vilikubaliana kufanya kazi kwa pamoja, lakini baada ya siku chache tu mvutano ulianza kati ya vyama hivyo.

Baadhi ya wafuasi wa chama cha Tshisekedi walianza kususia ushirikino huu, huku wakiwashutumu wafuasi wa chama cha Kabila kumzuia rais mpya kutekeleza ahadi zake.

Serikali ya DRC, ina mawaziri 60 ambapo 42 wanatoka katika chama cha Kabila huku 23 wakitoka katika muungano wa bwana Tshisekedi.