ZASPOTI
SHIRIKISHO la Soka la Afrika (CAF), limetangaza orodha ya wagombeaji wa urais wa shirikisho hilo katika uchaguzi utakaofanyika Machi, bila ya wagombea wa Wamisri wanaowania nafasi hiyo.


CAF ilitoa taarifa ikifunua orodha ya wagombea watano ambao wamewasilisha maombi ya kuwania jukumu hilo, akiwemo rais aliyesimamishwa Ahmad Ahmad.
Hivi karibuni, Ahmad alipigwa marufuku ya miaka mitano kutoka kwa shughuli zote zinazohusiana na mpira wa miguu baada ya kupatikana na hatia ya kutumia vibaya fedha za CAF kwa faida yake mwenyewe.


CAF ilisema kuwa mgombea wake ataangaliwa kwani uchunguzi kuhusu makosa yake bado unaendelea.
Wagombea watano wanaowania nafasi hiyo ni Ahmed Yahya (Mauritania),
Jacques Anouma (Ivory Coast), Patrice Motsepe (Afrika Kusini), Ahmad Ahmad (Madagascar), na Augustin Senghor (Senegal).


Shirikisho hilo pia limetoa majina ya walioteuliwa kuwania Ujumbe wa Kamati Kuu ya CAF, ambayo yalijumuisha maofisa 16 akiwemo Wadie Jary (Tunisia),Mustapha Ishola Raji (Liberia), Djibrilla Hima Hamidou (Niger) na Edwin Simeon- Okraku (Ghana).
Wengine ni Adoum Djibrine (Chad), Suleiman Waberi (Djibouti), Isayas Jira (Ethiopia),


Feizal Ismael Sidat (Mozambique), Elvis Raja Chetty (Seychelles), Maclean Cortez Letshwithi (Botswana) na Kanizat Ibrahim (Comoro), Patricia Rajeriarison (Madagascar) na Lawson Hogban-Latré-Kayti Edzona (Togo).


Kwa kuongezea, kuna wagombea watatu ambao wanahitaji uhakiki juu ya ustahiki wa kugombea kwao, ambao ni Mamadou Antonio Souare kutoka Guinea, Kameruni Seidou Mbombo Njoya, na Arthur De Almeida E. Silva kutoka Angola.
Uchaguzi umepangwa kufanyika Machi 12 huko Rabat, Morocco. (Goal).