LONDON, England
KLABU ya Brighton wamezipiga bao Manchester United na Atlanta United kwa makubaliano ya Moises Caidedo.

Caicedo anajiandaa kuondoka Independiente del Valle kwenda England huku akitarajiwa kupokea visa yake wiki hii.Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 19 tayari ni mchezaji kamili wa kimataifa kwa Ecuador na alikuwa mchezaji wa kwanza kuzaliwa katika karne ya 21 kuwahi kufunga katika Kombe la Dunia la CONMEBOL.

Yoso alitajwa kufukuziwa na Unietd ambayo imekuwa kwenye jitihada za kujijenga kwa ajili ya ushindani wa Ligi Kuu ya England.(TyC Sports).