NA SAIDA ISSA,DODOMA
HALMASHAURI ya wilaya ya Chamwino imeeleza kuwa imetega fedha kwa ajili ya mategenezo barabara zote korofi ikiwemo na madaraja yake yaliyoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha kwa hivi sasa.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Yarerd Swert alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, kuhusiana na wakazi wa kijiji cha Loje na Igunguli wilaya ya Chamwino kukosa mawasiliano kutokana na barabara hiyo kuwa mbovu na madaraja yake kukatika.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa hali halisi ya miundombuinu ya barabara na madaraja kwenye wilaya hiyo siyo rafiki kwa watumiaji wa vyombo vya moto na watembea kwa miguu baada ya kuharibika kulikotokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwa hivi sasa.
Alisema kuwa Halmashauri hiyo kwa mwaka huu imetega bajeti yake ya fedha bila kutaja kiasha chake, kwa ajili ya mategenezo hayo ya barabara ambazo ni korofi pamoja na madaraja ambayo hayapitiki kwa usafiri wa vyombo vya moto na hata kwa watembea kwa miguu.
“Ni kweli kuna barabara ambazo ndani ya halmashauri hii ya Chamwino ni mbovu kwa hivi sasa hii ni pamoja na baadhi ya madaraja kutopitika baada ya kuharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha kwa hivi sasa”
.
“Halmashauri imeshapitisha bajeti ya kutengeneza barabara zote korofi pamoja na madaraja,ila hajui wakala wa barabara vijijini (TARURA) wamefikia hatua gani kwa upande wao kwa ajili ya mategenezo yake”alisema.
Kwa upande wao wakazi wa kijiji cha Loje na Igunguli wilayani Chamwino wakizungumza na waandishi wa habari wamedai kuwa kwa hivi sasa hawana mawasiliano kati ya Loje na Igunguli kutokana na ubovu wa barabara na madaraja yaliyopo kukatika.
Mathayo Mazengo mkazi wa kijiji cha Loje alisema kuwa kutokana na ubovu wa barabara hiyo kwa hivi sasa shughuli zao zimesimama ikiwemo za kilimo na mvuvi ambao walio wengi wamekuwa kama sehemu wanayotegemea kujipatia kipato chao cha uchumi.
“Kijiji cha Igunguli kuna bwawa linalotumiwa kwa shughuli za uvuvi,hivyo hivi sasa hakuna kazi yoyote inayofanyika kutokana na kutopitika kwa barabara hiyo hali ambayo imewafanya vijana walio wengi kutokuwa na kazi pia hata kwa upande wa halmashauri yenyewe inakosa kukusanya mapato”alisema.
Naye Diwani wa wilaya ya Chamwino Tarafa ya Makangwa kata ya Loje Hild Kadunda alisema kuwa kwa hivi sasa hakuna mawasiliano kati ya Loje na Igunguli baada ya barabara kuwa mbovu pamoja na madaraja yaliyopo nayo kukatika.
Kadunda alisema kuwa kutokana na ubovu huo hivi sasa kwenye kata haye inakosa makusanyo yaliyokuwa yakipatikana kutokana na shughuli za uvuvi unaofanyika kwenye bwawa lililopo Igunguli hii ni pamoja na wananchi walio wengi kukosa kazi.
Hata hivyo ni mategemeo yake makubwa Halmashauri kwa kushirikiana na wakala wa barabara za vijijini (TARURA) wataitengeneza barabara hiyo ambayo ni muhimu kutokana na shughuli zinzofanyika za uvuvi ambao umekuwa ukiiletea halmashauri mapato kwa ajili ya maendeleo yake.