NA ASIA MWALIM

MADAKTARI na wauguzi wametakiwa kuwajibika katika utendaji wa kazi zao kwa kuwapatia huduma bora wagonjwa wanaofika kupata matibabu.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja, Sadifa Juma Khamis  alipokua akisikiliza changamoto za watendaji wa hospitali ya Kivunge wilaya ya Kaskazini Unguja.

Mkuu huyo alisema endapo wafanyakazi wa Hospitali na vituo vya afya mbalimbali nchini watafuata utaratibu, kanuni na sheria zililo wekwa itakua rahisi kwao kutoa huduma bora kwa jamii.

Aidha, alisema kufanya hivyo kutasaidia upatikanaji wa huduma za uhakika hospitali hapo ambapo wagonjwa wengi wa wilaya hiyo hufika kwa ajili ya kupata matibabu.

Alifahamisha kuwa Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwa kiasi kikubwa inapigania uboreshwaji wa huduma za afya nchini kwa kujengwa vituo vya afya, upatikaji wa dawa na vifaa ili kukidhi mahitaji ya wagonjwa na wananchi kwa ujumla.

“Endapo madakatri watafanya kazi zao kwa uadilifu kwa kuacha kufanya kazi kwa mazoea, lengo la Serekali litaweza kufikiwa Mjini na vijijini kote” alisema.

Kwa upande wake Meneja wa hospitali ya Kivunge Dhahai Humud Rashid ameiomba Serikali kuwapatia fedha za kutosha, ili kuweza kutatua matizo yanayowakabili hospitalini hapo na kuweza kupata maendeleo.

“Matatizo yanakuja baada ya wagonjwa kukosa huduma tukiboreshewa huduma tutaepushe migogoro isiyo ya lazima kwa wagonjwa wanaofika hapa” alisema.

Alifahamisha kuwa kuboreshwa kwa matibabu ni faraja kwa baadhi ya wogonjwa ambao wamekua wakikosa matibabu kwa wakati kutokana na upungufu wa baadhi vifaa hospitali hapo ambayo ni kimbilio la wananchi wengi.

Othman Juma Othman Daktari kitengo cha huduma ya Ex-ray ameiomba wizara ya Afya kuwaongezea wataalamu katika kitengo hicho kwani huduma hiyo bado ni tatizo hospitalini hapo.

Aidha aliomba Serekali kuwaendeleza kielimu madaktari wa hapo kwani kufanya hivyo kutasaidia kuondoa matatizo yojitokeza ndani ya huduma hiyo hospitalini ya kivunge.

Alishukuru Serikali kwa kwa kuwapangia mikakati maalum itakayoweza kukidhi mahitaji ya wagonjwa na wananchi kwa ujumla.

Hata hivyo, amewataka madaktari wa hospitali hiyo kushirikiana kwa pamoja, ili kufikia lengo lililokusudiwa katika kutoa huduma bora kwa wananchi .