MADRID, Hispania
KLABU ya Atletico Madrid wanakaribia kumsajili, Moussa Dembele kutoka Lyon, Diego Simeone amethibitisha.

Mshambuliaji huyo anatarajiwa kuhamia ‘Wanda Metropolitano’ kwa mkataba wa mkopo na chaguo la kumnunua, baada ya kuiambia Lyon anataka changamoto mpya.


Makubaliano hayo bado hayajakamilika, lakini, Simeone anaonekana kuwa na imani kuwa hatua hiyo itakamilika mapema kuliko baadaye.

“Bado haijathibitishwa, lakini, inasonga mbele sana,” Kocha huyo wa Atletico aliwaambia waandishi wa habari kabla ya mechi ya jana na Sevilla.

“Nitageuza kichwa changu kuelekea mchezo huo ambao ndiyo unayonivutia, na wakati kuna kitu [kwenye Dembele], nitatoa maoni.”Atletico inasemekana itaweza kumpata Dembele kwa ada ya euro milioni 33 endapo ataivutia kwa mkopo kabla ya msimu kumalizika.(Goal).