BEIJING,CHINA

KAMPUNI za Umoja wa Ulaya zilizoko China zinahofia kuhusu hatari mpya dhidi ya biashara zao, licha ya mkataba wa hivi karibuni wa uwekezaji uliosainiwa kati ya China na umoja huo.

Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa jana na ripoti  ya chama cha wafanyabiashara cha Umoja wa Ulaya mjini Beijing na pia taasisi ya China Merics iliyoko Berlin, wengi wana wasiwasi kwamba China na nchi nyengine zenye nguvu zinazidi kutengana, hali inayoweza kutatiza biashara ya kimataifa.

Walioiandika ripoti hiyo walisema kwamba hata chini ya utawala wa rais mteule wa Marekani Joe Biden, kuna uwezekano kwamba uhusiano kati ya China na Marekani utaendelea kuwa tete.

Mwishoni mwa mwaka jana, China na Umoja wa Ulaya walisaini mkataba wa uwekezaji baada ya miaka saba ya mazungumzo.