ZASPOTI
SHIRIKISHO la Soka la Rwanda (FERWAFA) kwa kushirikiana na Baraza la Uongozi la Dunia (FIFA), limepanga kujenga viwanja vitatu vyenye uwezo wa kukaa watu 3, 000 katika wilaya za Rutsiro, Rusizi na Gicumbi.
Mradi huo utaanza hivi karibuni kulingana na Shirikisho la Soka la Rwanda (Ferwafa) na unatarajiwa kugharimu fedha za Rwanda bilioni mbili.


Katibu Mkuu wa FERWAFA, Francois Regis Uwayezu, alisema shirikisho hilo pia litashirikiana na wilaya kujenga viwanja vya nyasi bandia katika wilaya nyengine tano kulingana na muono wao wa kuongeza miundombinu ya mpira wa miguu.


“Ujenzi wa viwanja vitatu utaanza hivi karibuni kwa kuwa mchakato wa ununuzi umekamilika. Tunazungumza pia na wilaya nyengine tano kujenga viwanja vyengine vitano vya mpira vya miguu ambavyo vinaweza kutumiwa na vijana wenye vipaji”.


“Lengo ni kujenga viwanja zaidi sio tu kwa fedha kutoka FIFA, lakini, pia na bajeti kutoka wilaya ambazo zitasimamia viwanja”, alisema, Uwayezu.
Inatarajiwa pia kuwa mara baada ya kukamilika, viwanja vitaongeza ukuzaji wa michezo na ukuzaji wa vipaji vya vijana katika ngazi ya chini kama sehemu ya mkakati mpana wa serikali wa kukuza michezo.


Ujenzi wa viwanja na nyasi bandia ilikubaliwa wakati wa kikao cha Mkutano Mkuu wa FERWAFA uliofanyika Mei 5, 2019, huko Musanze. Bunge lilipendekeza viwanja 10 vijengwe katika maeneo tofauti ya Rwanda.
Viwanja vitatu vitajengwa kwa awamu, kuanzia na kusawazisha maeneo na kujenga kuta za mzunguko kwa kila uwanja.


Wilaya ambazo zina viwanja vya nyasi bandia ni Huye, Rubavu, Muhanga, Kicukiro, Bugesera, Nyagatare, Ngoma, Nyarugenge, Rulindo na Rubavu.
Wilaya 20 zilizobakia bado hazina viwanja vya kisasa vya mpira wa miguu.
Uwanja wa Kitaifa wa Amahoro ndio uwanja mkubwa nchini una uwezo wa kuchukua watu 25,000, ukifuatiwa na uwanja wa Bugesera wenye uwezo wa kuchukua 15,000.


Uwanja wa Huye wenye (10,000), Uwanja wa Mkoa wa Kigali (7,000), uwanja wa Nyagatare unachukua 7000 na Ngoma ina uwezo wa kuchukua watu 6000 wakati Uwanja wa Umuganda unauwezo wa kukaribisha mashabiki 5,200.


Kwa sababu ya miundombinu mizuri, Rwanda iliidhinishwa kuandaa toleo la CHAN 2016 baada ya nchi hiyo kuandaa mashindano mawili ya vijana ya bara hili katika kipindi cha miaka mitatu, pamoja na Mashindano ya Vijana ya U-20 Afrika na 2009 na Mashindano ya U-17 mnamo 2011.(New Times).