ZASPOTI
KOCHA wa Bayern Munich, Hansi Flick, amesema, kipigo walichokumbana nacho kwenye mechi dhidi ya Borussia Monchengladbach, kimetokana na makosa waliyoyafanya kwenye kujilinda.
Mabingwa hao watetezi walichapwa magoli 3-2, licha ya kuongoza 2-0 kabla ya kibao kuwageukia kwenye uwanja wa Borussia-Park.


Mshambuliaji, Robert Lewandowski alifunga goli lake 20 la Bundesliga msimu huu kabla ya Leon Goretzka kuiwezesha Bayern kudhibiti pambano ndani ya dakika 26.
Lakini, magoli mawili ya Jonas Hofmann na Florian Neuhaus yakaibeba Gladbach iliyokuwa uwanja wa nyumbani.
“Tulitarajia mwisho tofauti wa mchezo huu na tulitarajia hilo, lakini, mwishowe tuliadhibiwa.


“Tulipoteza mpira bila ya ulazima mara tatu na wapinzani walikuwa na ufanisi mkubwa kumaliza nafasi hizo”, Flick aliwaambia waandishi wa habari baada ya mechi.
“Unaponiuliza jinsi ya kuzuia hilo, kwa upande mmoja lazima uzuie makosa, au ujiepushe nayo, na kwa upande mwngine unapaswa kufunika nafasi zako za chini mara mbili.


“Tulikumbana na hali kama hizo kwenye magoli yao mawili ya kwanza. Hofmann alikwenda chini kutoka kwenye kiungo na tukasogea mbele haraka na kufungua kati kati bila ya kufunika nafasi ya chini, na kwa goli la pili tulipaswa kuendelea kuziba nafasi hizo.


“Hiyo haifai kutokea na sio hali nzuri kuwa ndani, lakini, kushindwa, hata ikiwa ni Bayern Munich, ni sehemu ya mchezo. Katika kipindi cha pili timu ilijaribu kila kitu kupata matokeo mazuri, lakini, kwa bahati mbaya haikuweza kufanya kazi”.
mlinda mlango, Manuel Neuer sasa ameruhusu mechi 10 mfululizo za Bundesliga kwa mara ya kwanza katika taaluma yake, Bayern ikiachilia magoli 16 tangu kutoruhusu goli la mwisho dhidi ya Eintracht Frankfurt mnamo Oktoba 24.


Bayern wameruhusu magoli 24 kupitia mechi 15 kwenye ligi hiyo ya juu msimu huu, mengi zaidi ambayo wamesafirisha wakati huu wa kampeni ya Bundesliga tangu 1981-82.
“Nimesema mara kadhaa, tunafanya makosa mengi. Huwezi kukataa kwamba timu ilijaribu kushinda”, Flick, aliongeza:


“Ilibidi tupambane leo (juzi), tulijua utakuwa mchezo mgumu. Usisahau [Gladbach] ni timu ambayo ilicheza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya wapinzani wa juu na ikashinda, kwa hivyo tulihitaji utendaji huu wa timu na tulionyesha na isipokuwa hali hizi tatu.


“Lakini kwa kweli, haturidhiki na matokeo hayo. Sote tunajua tunahitaji kuonyesha umakini zaidi katika kazi yetu ya kujihami katika nyakati muhimu. Lazima tushughulikie nafasi za kina na hiyo ndiyo changamoto tuliyonayo, na tutaijiimarisha wiki zijazo”.
Bayern watarudi uwanjani dhidi ya timu ya Bundesliga 2 ya Holstein Kiel katika Kombe la DFB-Pokal keshokutwa.(AFP).