NA MBARAKA KAMBONA
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul, amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuhakikisha kuwa ndani ya siku 7 anamlipa Mkandarasi anayejenga Machinjio ya Vingunguti shilingi bilioni 5 anazodai ili aweze kukamilisha ujenzi huo.
Gekul alitoa agizo hilo alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa machinjio hayo yaliyopo jijini Dar es Salaam, ambapo alisema kuwa hali za machinjio nyingi kwa sasa sio nzuri, Wanyama wanachinjwa katika mazingira machafu na sio salama kwa walaji huku akisema machinjio hayo ya Vingunguti yatakuwa mkombozi kwa wananchi wa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.
“Kwa hiyo Mkurugenzi hakikisha ndani ya siku saba kuanzia leo tarehe 8 (juzi) unamlipa Mkandarasi ili kazi hii ikamilike kama ambavyo Rais, Dk. John Magufuli alivyoagiza,” aliagiza Gekul.
Gekul aliendelea kusisitiza kuwa kukamilika kwa ujenzi huo ni lazima uende sambamba na ununuzi wa magari kwa ajili ya kubebea nyama na kuzisambaza katika mabucha yaliyopo jijini Dar es Salaam kwani haitapendeza kuwepo kwa machinjio hayo mazuri halafu nyama ziwe zinabebwa kwenye pikipiki. Aliongeza kuwa ili kuhakikisha machinjio hayo yanapata Wanyama wazuri na salama kwa ajili ya walaji, wataboresha mnada wa machinjio ya Pugu ili wanyama watakao