BEIRUT, LEBANON
GHASIA zimepamba moto nchini Lebanon baada ya kifo cha mtu mmoja aliyeshiriki kwenye maandamano ya kupinga hali mbaya ya maisha iliyosababishwa na mgogoro mkubwa wa fedha ambao haujawahi kushuhudiwa nchini humo.
Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi kuwakabili vijana waliokuwa wanawatupia mawe katika mji wa Tripoli, kupinga kuuliwa kwa kijana huyo kwa kupigwa risasi na polisi.

Kijana huyo aliyeuawa alikuwa na umri wa miaka 30. Watu zaidi ya 200 ikiwa pamoja na polisi 26 pia walijeruhiwa kwenye maandamano hayo yaliyoingia siku ya nne.
Watu hao walijikusanya kwenye makaazi ya wanasiasa wa ngazi za juu na kuchoma moto magari.