LONDON, England

KOCHA Mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kuwa vijana wake walistahili kushinda kwa kuwa walijituma mwanzo mwisho wakiwa darajani.

Manchester City ilishinda mabao 3-1 dhidi ya Chelsea ya Frank Lampard wakiwa ugenini ndani ya Stamford Bridge kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.

Mabao ya City yalifungwa na Likay Gundogan dakika ya 18, Phil Foden dakika ya 21 na Kevin De Bruyne dakika 34, huku lile la kufutia machozi kwa Chelsea likifungwa dakika za lala salama na Callum Hudson-Odoi dakika ya 90+2.

Ushindi huo unaifanya Manchester City kuwa nafasi ya tano na pointi zake kibindoni ni 29 huku Chelsea ikiwa nafasi ya nane na pointi 26.

Guardiola amesema:”Haikuwa kazi rahisi tukiwa ugenini na tumeanza 2021 kwa kupata pointi tatu ni jambo la furaha kwetu na wachezaji kiujumla wanastahili pongezi,” .