NA TIMA SALEHE,DAR ES SALAAM

MSANII wa Muziki wa Kizazi kipya, Harmonize ameahidi kuachia wimbo wa kwanza kwa mwaka 2021 ambao atamshirikisha msanii chipukizi Anjella Tz.

Atafanya kazi hiyo mpya na msanii huyo kwa lengo la kumsaidia kutimiza malengo yake ya muziki.

Akizungumza kupitia video hivi karibuni Harmose alisema amependa kufanya kazi na msanii huyo ambaye ana sauti nzuri.

Harmonise ni miongoni mwa wasanii wakubwa Tanzania ambao wanauwakilisha vyema muziki wa Afrika na nje ya Afrika.