BANGUI, AFRIKA YA KATI
MAHAKAMA ya kimataifa ya jinai ya ICC, imesema kuwa imemtia mbaroni aliyekuwa kamanda wa kundi la uasi la Seleka huko Jamhuri ya Afrika ya Kati linaloshukiwa kutekeleza uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, ICC ilisema kuwa Mahamat Said Abdel Kain alijisalimisha Jumapili na kukamatwa kufuatia hati ya iliotolewa Januari 7, 2019 kutokana ukatili uliotekelezwa 2013.
Hata hivyo tarehe ya kufikishwa mbele ya mahakama mjini Hague haijatangazwa.
Ukamataji huo ulifanyika wakati kukiwa na hali ya taharuki nchini humo kufuatia mapigano kati ya jeshi la serikali likiungwa mkono na Russia na Rwanda na waasi wanaopinga ushindi wa rais Faustin Archange Touadera kufuatia uchaguzi wa Decemba 27.
Taifa hilo limekuwa likishuhudia machafuko tangu muungano wa waasi wa kiislamu kutoka upande wa kaskazini kwa jina Seleka walipochukua madaraka Machi 2013.
Utawala wao ulipelekea wapiganaji wa kikristo kwa jina anti balaka ambao wengi wa viongozi wao wanakabiliwa na mashihtaka mbele ya ICC.