ZASPOTI
RAIS wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino, ametua nchini Cameroun kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika (CHAN), 2020.
Rais wa muda wa CAF, Constant Omari alikutana na Infantino wakati wa kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nsimalem kabla ya kuanza kwa michuano hiyo ya wachezaji wanaocheza soka nyumbani Afrika.
Omari aliandamana na Rais wa Shirikisho la Soka la Cameroun, Seydou Mbombo Njoya na nguli wa mpira wa miguu Afrika, Samuel Eto’o walipokutana na Infantino katika ziara yake ya kwanza katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati.
Infantino alihudhuria kikao cha Kamati ya Utendaji ya CAF kabla ya kushuhudia hafla ya kumtawaza, Issa Hayatou kama Rais wa Heshima wa CAF.
Rais huyo wa FIFA alikuwepo katika Uwanja wa Ahmadou Ahidjo jijini Yaounde kushuhudia mechi ya ufunguzi ya CHAN kati ya Cameroun na Zimbabwe.(Goal).