NCHI nyingi barani Ulaya kwa wakati huu zinapitia kipindi cha awamu ya pili ya kusambaa kwa virusi vya corona, huku baadhi ya nchi zikitekeleza masharti magumu ya kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo.

Hata hivyo, kuna habari njema kwa tayari wataalamu wa afya wamevumbua chanjo ya corona, huku baadhi ya nchi kama Uingereza zikiidhinisha utumiwaji wa chanjo hiyo.

Hospitali nchini Uingereza ziko kwenye maandalizi ya mwisho tayari kwa ajili ya utoaji wa dozi ya chanjo virusi vya corona kwa kile ilicholeza kwamba wadhibiti wa viwango wameidhinisha matumizi ya chanjo ya Pfizer/BioNTech kutumika.

Lakini wakati wengi wakitaka kudungwa haraka sindano ya chanjo ya corona, baadhi wanawasi wasi juu ya kuingiza kitu wasichaokifahamu ndani ya miili yao.

Tunafahamu vipi chanjo hii ni salama? Hili ndio swali la kwanza na la muhimu ambalo wanasayansi hujiuliza wanapoanza kutengeneza chanjo mpya au dawa mpya.

Majaribio ya usalama wake huanza katika maabara, kwa majaribio na utafiti unaofanywa kwa seli na wanyama, kabla ya kuhamishia majaribio hayo kwa binadamu.

Kanuni ni kuanza kidogo na kuhamia katika hatua nyingine tu pale wanapoona kuwa hakuna hofu za usalama.

Majaribio yana umuhimu gani? Data salama kutoka kwenye maabara zinapokuwa nzuri, wanasayansi wanaweza kuangalia kwamba chanjo au matibabu ni ya ufanisi pia.

Hii inamaana kuwa kwa idadi kubwa ya watu wanaojitolea kufanyiwa majaribio ya chanjo takriban 40,000 ndio walioshiriki katika majaribio ya chanjo iliyovumbuliwa na kampuni ya Pfizer/BioNTech.

Katika majaribio, nusu ya watu hupewa chanjo na wengine hupewa nusu dozi ya kupunguza makali ya ugonjwa. Watafiti na washiriki huwa hawaambiwi wako katika kundi gani, mpaka baada ya matokeo kufanyiwa tathmini, ili kuepusha upendeleo wa matokeo fulani katika tathmini.

Kazi yote na matokeo huwa yanaangaliwa na kuhakikiwa na taasisi huru. Majaribio ya chanjo ya corona yamefanyika katika kwa kasi kubwa, lakini hayakuvuka hatua hizi.

Chanjo ya corona ya Oxford/AstraZeneca ilicheleweshwa kwa makusudi katika awamu moja ili kuchunguza ni kwanini mshiriki mmoja kati ya maelfu ya watu alikufa. Utafiti wake uliendelea pale ilipogundulika wazi kuwa kifo chake hakikuhusiana na chanjo.

Ni nani anayeidhinisha chanjo au tiba? Idhini itatolewa tu kwa chanjo pale wadhibiti wa serikali, mamlaka ya uangalizi wa ubora wa dawa na bidhaa za afya (MHRA), itakapofurahia usalama na ufanisi wake.

MHRA ni sehemu ya wizara ya afya na ina wafanyakazi zaidi ya 1,200. Mkuu wake dokta June Raine, ambaye amekuwa akifanya kazi kwa muda mrefu katika udhibiti wa viwango vya dawa.

Alisema, “Umma unaweza kuwa na imani kabisa kwamba viwango tulivyovifanyia kazi ni sawa na vile vya kote duniani”, alisema.

Uchunguzi wa mara kwa mara juu ya chanjo utaendelea ili kuhakikisha hakuna madhara mengine au hatari za muda mrefu. Kama mtu yeyote atashuku kuwa anaumwa athari zitokanazo na chanjo, anaweza kuripoti katika taasisi ya MHRA.

Wataalamu huru wa kamati ya pamoja kuhusu chanjo huamua ni vipi chanjo inaweza kutolewa kwa ubora zaidi na ni nani anayepaswa kuchanjwa kwanza

Kamati ya JCVI, ambayo ina wajumbe takriban 20 ambao ni wataalamu wa chanjo, inaongozwa na Profesa Andrew Pollard, anayefanya kazi katika Chuo Kikuu cha Oxford.

Nini kilichomo ndani ya chanjo ya Covid? Kuna aina nyingi tofauti za chanjo za corona zinazotengenezwa baadhi yake zina virusi vyenyewe vilivyosababisha maradhi hayo.

Chanjo ya Oxford AstraZeneca inatumia virusi vusivyo na madhara ambavyo vimefayiwa mabadiliko ya muonekano wake ili kufanana zaidi na kama Sars-CoV-2 – virusi vinavyosababisha Covid-19.

Chanjo za Pfizer/BioNTech na Moderna hutumia aina fulani ya urithi ya jeni kusababisha utendaji wa kinga ya mwili, na huitwa chanjo za mRNA. Hizi hazibadili seli za binadamu. Hutoa tu maagizo kwa mwili ili ujenge kinga dhidi ya Covid.

Baadhi ya dozi za corona huwa zina protini kutoka kwa virusi vya corona. Chanjo wakati mwingine huawa na viungo, aluminiam, ambayo hufanya chanjo kuwa thabiti au yenye ufanisi zaidi.

Je chanjo itanifanya niwe mgonjwa? Hakuna ushahidi kwamba kiungo chochote kilichowekwa ndani ya chanjo kinaweza kuwa na madhara kinapotumiwa kwa kiasi kidogo kama ilivyo.

Chanjo hazikupatii ugonjwa. Badala yajke, zinafundisha mfumo wetu wa kinga ya mwili kutambua na kupambana na maambukizi ambayo zimetengenezwa kupambana dhidi yake.

Baadhi ya watu huugua kwa dalili ndogo, kama vile maumivu ya misuli au kupanda kidogo kwa joto la mwili, baada ya kuchanjwa.

Profesa Sir Munir Pirmohamed, ambaye anashauri taasisi ya MHRA, alisema kuwa bado hawajatambua athari yoyote mbaya wakati wa majaribio ya chanjo ya Pfizer/BioNTech.

Alisema “Athari zilizojitokeza zaidi ni kidogo na za muda mfupi, mara nyingi hudumu kwa siku moja au mbili, sawa na athari unazozipata unapopata chanjo nyingine yoyote ile “. Aliongeza kuwa MHRA ina mkakati “wa kufuatilia kwa karibu “usalama wa chanjo.

Kuwa makini kuhusu taarifa za kupotosha za chanjo za corona zinazosambazwa katika mitando ya kijamii. Taarifa hizo haizambatani na ushahidi wa kisayansi (au zinajumuisha ukweli na upotoshaji).

Ni sawa mtu aliyekuwa na Covid kupata chanjo? Watu watapewa chanjo ya corona hata kama waliwahi kuugua uganjwa huo. Hii ni kwasababu kinga asilia huenda imeathiriwa na chanjo hii itatoa ulinzi zaidi.

Muongozo kutoka afya ya umma ya Uingereza unasema hakuna hofu ya usalama wa watu waliowahi kuambukizwa virusi vya corona kupewa chanjo, lakini watu ambao kwa sasa wanaugua Covid-19 hawastahili kupewa chanjo hadi wapone.

Ikiwa kila mtu atapewa chanjo basi sina haja ya kuwa na hofu? Kuna ushahidi mkubwa wa kisayansi unaobaini kuwa chanjo ndio kinga mudhubuti dhidi ya magonjwa ya kuambukizi.

Chanjo ya corona ina uwezo wa kuwakinga watu kupata maambukizi na hivyo basi kuokoa maisha. Dozi za kwanza zitapewa watu walio katika hatari zaidi kama wazee ambao huenda wakawa wagonjwa zaidi wakiugua.

Haijabainika chanjo hiyo inatoa ulinzi wa wa kutosha kuwaepusha watu dhidi ya kusambaza ugonjwa wa corona ikiwa itafanikiwa kufanya hivyo, kuwapa chanjo watu wengi kutatokomeza ugonjwa huo.