NA FATUMA KITIMA, DAR ES SALAAM

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya wiki ya sheria yatayofanyika Februari 1 katika viwanja Chinangali mjini Dodoma .

Pia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye matembezi ya wiki ya sheria Januari 24, mwaka huu, ambayo  yataanza kwenye mahakama kuu ya Tanzania hadi  katika viwanja vya Nyerere Square jijini humo mjini Dodoma.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma, alisema wiki ya sheria itaanza Januari 23 hadi 29, mwaka huu yatayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Dodoma.

Alisema maonyesho hayo yataenda sambamba na maika 100 tangu kuanzishwa kwa mahakama Kuu ya Tanzania, ambapo kauli mbiu ni miaka 100 ya Mahakama kuu mchango wa Mahakam katika kujenga nchi inayozingatia uhuru haki amani ,ustawi wan chi kati ya 1920 mpaka 2020 .

Alieleza kauli mbiu hiyo inalenga kuonesha ufanisi wa Mahakama na utoaji haki kwa miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Mahakama  kuu ya Tanzania.

“Sambamba na maonesho hayo utaji wa elimu kwa umma utafanyika katika kanda, mikoa hivyo tunaomba wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuweza kupata elimu mbalimbali ya masuala ya sheria “alisema

Alifafanua elimu itayotolewa ni pamoja na utaratibu wa kufungua mashauri kwa njia za kawaida, lakini kama mnavyofahamu tumeanza karne ya 21 kufungua mashauri kwa njia ya mtandao ni njia nzuri kwa wanannchi kufahamu njia hiyo mpya. Vile vile, wataweza kufahamu njia zinazotumika kuendesha mashauri kutoka kwa wahusika kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo sheria za watoto, ndoa na talaka