Lengo kuishi kwa mani, upendo na mshikamano

NA SHEIKH KAMAL ABDUL-MU’TY ABDUL-WAHED

KATIKA kutekeleza majukumu yake ya kueneza dini sambamba na kutoa mafunzo ya dini hiyo hapa Tanzania, hivi karibuni Kituo cha kiislamu ya Misri ilifika Mjini Morogoro na kutoa mafunzo ya dini hiyo.

Mkurugenzi wa kituo cha Kiislamu cha Misri, tawi la Dar es Salaam, Tanzania Sheikh/ Kamal Abdul-Mu’ty Abdul-Wahed akifungua mafunzo hayo, alisema lengo la kituo hicho ni kutoa mafunzo mbalimbali yanayohusina na dini jambo ambalo linawakumbusha waumini juu ya kutenda mema na kuacha mabaya.

“Wakati umefika sasa kwa waislamu kuhakikisha wanafuata miongozo ya Allah (S.W) kwa kuacha mkatazo yake na kutenda mema na ndio maana tukaamua kutoa semina, khutba, darsa na daawa kwa ajili ya kueneza fikra sahihi na kuachana na mambo maovu”, alisema.

Sheikh/ Abdul-Mu’ty alisema anafurahia kuona kwamba taaluma ya dini ya kiislamu imekuwa kubwa hasa sehemu za mikoani jambo ambalo linaleta ushirkiano mkubwa katika jamii.

Sambamba na hilo lakini aliwashukuru viongozi wa mkoa huo kwa kuwapa ushirikiano mkubwa katika kufanikisha mafunzo hayo.

Pia, alisisitiza nia ya Kituo cha Kiislamu cha Misri ni kuimarisha ushirikiano na taasisi mbalimbali za elimu na kidini kwa ajili ya kueneza elimu yenye kuwanufaisha watanzania wote.

Nae Sheikh/ Mohammed Abdul-Fattah Bayoumi, ambae ni mjumbe wa Kituo cha Kiislamu cha misri, Dar es Salaam, akiwasilisha mada katika mafunzo hayo juu ya “Wito wa Uislamu kwa usamehevu wa kidini na kukataa umadhehebu wala mizozo ya kidini”, ambapo alisisitiza kuwa Uislamu ni dini inavyohimiza kudumisha amani, kusameheana, kuishi kwa utulivu katika jamii.

“Nawasisitiza juu ya kulitilia mkazo suala la amani katika jamii na kuishi kwa kupendana kwa watu wote bila ya kujali dini, rangi, jinsia, tabaka, kabila au vingenevyo.

Pia, Sheikh Bayoumi, aliwataka maimamu na viongozi wa dini kutekeleza wajibu wao katika kuwaongoza waumini na kuhakikisha amani na utulivu kupitia uwajibikaji uliotukuka.

“Jamii ya kiislamu inahimiza kusameheana na kuvumiliana, pamoja na kuishi kwa amani na upendo jambo ambalo linamfaa mja dunaini na akhera”, alisema.

Sambamba na hilo, aliwataka maimamu na masheikhe na wakuu wa kila jamii kulitilia mkazo suala la elimu ya dini ili kuleta maendeleo na mafanikio ya umma wao na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Sheikh Aref Al-Nahdi, mkurugenzi wa Taasisi ya Kiislamu mkoani Morogoro “Islamic Foundation” alikishukuru kituo cha Kiislamu cha misri kwa juhudi zak za kueneza maadili mema ya dini ya kiislamu.

“Ni wajibu wetu kujenga jamii bora yenye misingi ya kusameheana, kupendana na kuhurumiana”, alisema.

Vile vile, Sheikh Al-Nahdi, alieleza kuwa semina hiyo ni muhimu mno kwa kuwa wengi wa vijana wa siku hizi wanakosa utamaduni wa kusameheana, wengine wameathirika vibaya kwa hotuba za chuki na kujisukuma kutenda maovu.

Mada nyeingine iliowasilishwa katika mafunzo hayo ni “Uzalendo na kuishi pamoja kwa amani” ambapo alisisitiza kuwa sheria ya kiislamu inawahimiza waisalmu wawe wazalendo wa kweli na kuwataka kutekeleza majukumu yao kwa ajili ya kujenga jamii bora yenye amani na utulivu.

Sheikh Eslam, ambae ni mjumbe wa kituo cha kiislamu cha Misri alifafnua na kusema kuwa vijana ni mustakbali wa umma wanatakiwa kuwajibikia ili watoe sura nzuri kuhusu dini yao na taifa lao kwa ujumla.

Mapema Sheikh Al-Hadi Mussa, Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, ambae alikuwa mgeni rasmi katika mafunzo hayo alitoa neno la shukrani na kusema kuwa “Uislamu ndio dini ya Amani” ambayo imekusanya vigezo mbalimbali vinavyosisitiza haki na wajibu za kila mmoja katika ulimwengu wa sasa.

“Pamoja na tofauti za kisasa zilizopo ipo haja ya kuhakikisha amani na usalama wa taifa na kimataifa unafuatwa ikiwa ni pamoja na kuvumiliana na kueneza tabia zinazomfurahisha muumba wetu”, alisema.

Katika mafunzo hayo yalihudhuriwa na Sheikh Daudi Nkuba, Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Morogoro (ASP) ambapo aliwataka maimamu kuwaelekeza vijana na jamii kwa jumla kwenye maadili ya usamehevu na upole ili kuleta maendeleo ya dhati.

Nkuba alitoa shukurani kwa Kituo cha Kiislamu cha Misri kwa juhudi zake za kuhimiza amani na utulivu kupitiaa taaluma ya dini.

Pamoja na mambo mengine lakini mafunzo hayo yalikuwa na lengo la kuikumbusha jamii juu ya kuishi kwa upendo, amani na mshkamano jambo ambalo litawaletea maendeleo wao binafsi na taifa kwa ujumla.

Mafunzo hayo yalihudhuriwa na mashehe, maimamu vijana na walimu wapatao 260 kutoka wilaya mbalimbali za mkoa wa Morogoro.