LONDON, England
JURGEN KLOPP amebaini wachezaji wake wa Liverpool watafanya mazoezi mengi kabla ya pambano lao dhidi ya Manchester United mnamo Januari 17.
Ratiba ngumu ambayo Klopp amekuwa akiikosoa waziwazi , ambayo haitowi nafasi kwa timu za ligi kuu kupumzika.
Baada ya ushindi wa Ijumaa usiku 4-1 dhidi ya Aston Villa katika pambano lao la raundi ya tatu ya Kombe la FA huko Villa Park, Liver sasa wana siku tisa kujiandaa na mchezo wao wa ligi na United.
Sadio Mane alifunga bao baada ya dakika nne tu kabla ya Louie Barry kusawazisha na kufanya 1-1 wakati timu hizo zilipokwenda mapumziko nguvu sawa.
Liverpool wamekuwa hawana matokeo mazuri ligi ya kuu katika michezo mitatu iliyopita.
Wameiruhusu United kutengeneza nafasi ya kuwakaribia kwenye msimamo, na kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer kuweza
kwenda juu ya msimamo ikiwa wataifunga Burnley Jumanne.
Lakini Klopp anafurahiya mapumziko kwa timu yake na alikiri watakuwa wakitafuta mechi nyingi za kujipima nguvu kujiandaa kukabiliana na Mashetani Wekundu.