NA NASRA MANZI

TIMU za KMKM wanaume na JKT wanawake zimefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya kombe la mapinduzi kwa mpira wa mikono (Handball).

Mashindano hayo yalijulikana kwa jina la umoja mapinduzi cup yalikuwa wakifanyika katika uwanja wa Migombani jeshini.

KMKM wanaume ilifanikiwa kutwaa ubingwa huo baada ya kuvuna pointi sita.

Mshindi wa pili alikuwa JKU wanaume kwa kupata pointi nne wakati mshindi wa tatu alikuwa JKT kutoka Tanzania bara kwa kupata pointi mbili.

Kwa upande wa wanawake mshindi wa kwanza alikuwa JKT baada ya kuvuna pointi nne akifuatiwa na JKU aliyepata pointi mbili,wakati mshindi wa tatu KMKM hakupata pointi hata moja.

Kwa upande wa vijana timu ya Mwanakwerekwe wanaume ilipata ubingwa kwa kupata pointi nane,wakati mshindi wa pili alikuwa Victori akiwa na pointi sita na mshindi wa tatu Wete alikuwa na pointi nne

Kwa upande wa wanawake mshindi wa kwanza Victori aliyevuna pointi nne,akifuatiwa na skuli na Miwani wakiwa na pointi mbili ,huku mshindi wa tatu Wete Pemba ambaye hakupata pointi.